Habari za Punde

TAMBWE AISHUSHA TOTO AFRICAN, AIPA UBINGWA YANGA UWANJA WA TAIFA

 Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akishangilia baolake ambalo lilikuwa ni pekee katika mchezo wao dhidi ya wadogo zao Toto Africa wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa Amis Tambwe katika dakika 72.
Kwa ushindi huo sasa Yanga wamejihakikishia ubingwa baada ya kufikisha jumla ya Pointi 68 ambazo wapinzani wao Simba hata wakishinda mchezo wao uliobaki bado Yanga watakuwa wakibebwa ba wastani mkubwa wa mabao ya kufunga huku wakiwa bado wana mchezo mmoja mkononi dhidi ya Mbao Fc utakaopigwa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 Amis Tambwe akifunga bao hilo katika mchezo huo uliokuwa na upinzani mkubwa
 Nahodha Niyonzima akimpongeza Amis Tambwe baada ya kutupia bao hilo.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe, ameipa ubingwa Yanga wa Ligi Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo.
*************************************
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa, Amis Tambwe, alifunga bao pekee dakika ya 72 kwa mpira wa kichwa akiunganisha krosi ya beki wa kulia, Juma Abdul dhidi ya Toto Africans ya Mbeya kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezaji huyo wa zamani wa Simba, alifunga bao hilo kwa ustadi mkubwa akitokea mbali ya eneo la hatari, kabla ya kumzidi maarifa mmoja wa mabeki wa Toto Africans.
Toto Africans, ilitaka kuchelewesha ubingwa wa Yanga, baada ya jana kuing'ang'ania timu hiyo muda mrefu wa mchezo.
Kwa matokeo ya jana, Yanga imefikisha pointi 68 ikiwa kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mbele ya watani wao wa jadi Simba.
 Shabiki wa Yanga akishngilia kwa staili ya kula Samaki mara tu baada ya Tambwe kutupia bao hilo. Shabiki huyu huwa na staili tofauti tofauti za kushangilia kulingana na timu inayo kuwa ikicheza dhidi ya timu yake ya Yanga, ambapo majuzi aliibuka uwanjani hapo akiwa na Mahotpot mawili yakiwa na kipolo cha ubwabwa maharage, siku za nyuma alishaibuka uwanjani hapo akiwa na Msumeno wakati Yanga ikicheza na Mbao Fc na nyinginezo,
*********************************************
Simba iko nafasi ya pili ikiwa na pointi 65 na imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Mwadui Shinyanga, utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu hiyo imetwaa ubingwa kwa kuwa Simba ikishinda mchezo dhidi ya Mwadui itafikisha pointi 68 sawa na wapinzani wao. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Endapo Yanga itafungwa na Mbao katika mchezo wa mwisho, Simba itakuwa mabingwa ikiwa itashinda mabao zaidi ya 10 dhidi ya Mwadui.
Hata hivyo, Yanga ina uwiano mzuri wa idadi ya mabao ambayo yanaipa fursa ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo.
Uwanja wa Taifa ulipambwa na rangi za njano na kijani zilizovaliwa na mashabiki wa klabu hiyo kutoka Makutano ya Mtaa wa Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Muda mfupi baada ya mpira kumalizika, wachezaji wa Yanga wakiongozwa na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' walicheza sebene uwanjani kusherehekea ushindi huo.
Michuano ya Ligi Kuu Tanzania msimu huu inatarajiwa kumalizika Jumamosi wiki kwenye viwanja tofauti nchini ambapo timu 16 zitateremka uwanjani kuwania pointi tatu.
Yanga imebakiwa na mchezo mmoja wa kumaliza Ligi Kuu ambao itakuwa ugenini kupepetana na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Awali, Abdul alianza kutoa presha kwa Toto Africans, baada ya kupiga mpira wa krosi, lakini ulikosa mfungaji.
Abdul, aliyekuwa akicheza nafasi ya beki wa kulia, alipanda mbele kusaidia mashambulizi na dakika ya tatu alipiga mpira ulishindwa kuwekwa wavuni na mchezaji wa kimataifa, Obrey Chirwa.
Chirwa, alikosa bao dakika ya 13 baada ya kushindwa kuunganisha mpira wa faulo uliopigwa na Abdul, baada ya kupiga shuti nje. Libero wa Yanga, Vincent Bossou, alikosa bao dakika ya 16.
Toto Africans ilijipanga na kufanya shambulizi la kushitukiza dakika ya 23 kupitia kwa beki, Lusajo Lerien.
Nahodha wa Yanga katika mchezo wa jana, Haruna Niyonzima, alikosa bao dakika ya 56 kwa shuti lake kutoka nje kidogo ya lango.
Katika dakika 45 za pili kocha wa Yanga, George Lwandamina, alimtoa Juma Mahadhi na kuingia Deus Kaseke ambaye aliongeza mashambulizi na kuwapa kazi ngumu mabeki wa Toto Africans.
Kipindi cha pili Yanga ilifanya mashambulizi makali mfululizo kutokea wingi za kulia na kushoto.
Mabeki Abdul na Mwinyi Haji, aliyekuwa akicheza upande wa kushoto, walifanya kazi kubwa ya kupira mipira ya krosi.
Yanga ilifanya shambulizi kali na nusura ipate bao dakika ya 85, baada ya Deus Kaseke, kupiga shuti lililodakwa kwa ustadi na kipa wa Toto Africans, David Kisu.
*************************
KIKOSI CHA YANGA: Benno Kakolanya, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Haruna Niyonzima/Justine Zulu, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe na Geofrey Mwashiuya/Emmanuel Martin.


KIKOSI CHA TOTO AFRICAN: David Kisu, Lusajo Lerient, Mohammed Soud/ Ramadhani Waziri, Hamimu Abdul, Ramadhani Malima,  Yusuf Mlipili, Carlos Protas, Hussein Kadanga, Waziri Junior, Juvenary Pastory/Mhando Robert na Jafari Mohammed.
 Chirwa akipambana na mabeki wa Toto African 
 Gooooooooooooooo
 Hatari langoni kwa Toto African
 Deus Kaseke akichuana na beki wa Toto African
 KIpa wa Toto African akiruka kupangua mpira wa hatari langoni kwake...
 Mashabiki wa Yanga wakiwa katika sare maalum kuomboleza kifo cha shabiki mwenzao
Wachezaji wa Yanga wakishangilia

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.