Habari za Punde

TFF YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA WILD AID KUPIGA VITA UJANGILI WA WANYAMA PORI

Rais wa TFF, Jamal Malinzi akibadilishana mkataba huo na Ofisa wa Wild Aid Tanzania, Lily Massa, wakati wa hafla hiyo fupi ya kusaini mkataba. 
******************************************************
Na Asia Gamba Dar
SHIRIKISHO la soka nchini TFF kupitia Rais wake, Jamal Malinzi leo limesaini mkataba wa ushirikiano na taasisi binafsi ya Wild Aid Tanzania inayojihusisha na kupiga vita ujangili dhidi ya wanyama pori.
Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Courtyard, Oysterbay, Dar es Salaam, Malinzi alisema ushirikiano huo utaanza kufanyiwa kazi kupitia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
“Kama mnavyofahamu, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, pamoja na kutangaza, moja ya majukumu makubwa ya TFF ni matatu, kuendeleza, kuitangaza nchi na kuongoza mchezo kwa mujibu wa sheria, lakini pia kwa upande wa jamii huwa tunapenda kujihusisha na mambo mbalimbali,”amesema.
Malinzi amesema huo ni mwendelezo tu wa mahusiano mazuri kati ya TFF na Jamii na Wild Aid itautumia mpira wa miguu kikamilifu katika kampeni zake za kutunza wanyama pori. 
Kwa upande wake, Ofisa wa Wild Aid Tanzania, Lilly Massa amesema kwamba wamefurahi kwa kuingia kwenye mahusiano na TFF na mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla.
Alisema tayari wapo mahusiano na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet anayecheza Marekani na mwanamuziki Ali Kiba hivyo kuongezeka kwa TFF ni hatua nyingine nzuri kwao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.