Habari za Punde

TRL KUWAPELEKA JELA ABIRIA WANAONING'INIA NJE YA MABEHEWA


Meneja Usafirishaji abiria wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Iddi Mzugu, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye mkutano uliofanyika Ofisi za TRL jijini Dar es Salaam, leo wakati wakitoa tamko kwa watumiaji wa huduma za Treni za abiria kuhusu kuzingatia sheria baada ya moja ya gazeti nchini kuripo kuning'inia kuwa abiria katika usafiri huo hivi karibuni. Katikati ni Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi, Frank Gadau (kulia) ni Meneja Usalama na Ulinzi wa Reli, Marko Gukwi.
*******************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
WATUMIAJI  wa huduma za usafiri wa Treni za abiria za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya usafiri huo ili kuepuka sdhabu ya kufungwa jela miezi sita au faini ya Sh. 50,000.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Uongozi wa TRL, umesema kuwa matumizi ya usafiri wa abiria unasimamiwa na sheria, kanuni, taratibu na masharti maalum, mojawapo ikiwa ni kutodandia mabehewa baada ya milango kufungwa.
TRL wametoa taarifa hiyo baada kuonekana kushamiri kwa vitendo vya uvunjifu wa taratibu za usalama za usafiri wa Treni, ambapo aina hii ya uvunjaji wa matumizi yasiyo salama kwa mwaka jana mwezi agosti yalisababisha mtu mmoja kupoteza maisha baada ya kugongwa na geti la lango la kuingilia Treni Stesheni.
Aidha imeelezwa kuwa marehemu huyo alikuwa akining'inia nje ya behewa wakati Treni ya Pugu majira ya jioni ikiingia ndani ya eneo la Kituo cha Dar es Salaam.
Uongozi wa TRL umefafanua kuwa tofauti ya usafiri wa basi ni kwa vile Kondakta anaweza kusimamisha basi ili kumshusha abiria anayeni'nginia nje lakini kwa Treni haiwezekani kufanyika kirahisi.
Uongozi wa TRL umetoa wito kwa watumiaji wa usafiri huo na wananchi kwa ujumla kufuata masharti ya usafiri wa Treni za Jiji na hasa kwa wale wanaotumia usafiri wa Treni ya Pugu, ili kuepuka maafa na kuchukuliwa hatua za kisheria ambazo zitampelekea mhusika wa kosa kwenda jela miezi sita ama kulipa faini.
Kwa upande wa Kikosi cha Polisi Reli, kimeanza Operesheni ya kuwadhibiti abiria ambao hawataki kufuata sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya usafiri salama wa Treni na hasa kwa kuning'inia nje ya mabehewa wakati treni ikiwa katika mwendo. 
Pia Operesheni hiyo itahusisha kuwafikisha mahakamani wasafiri wote watakaokamatwa wakienda kinyume na taratibu za usalama wa usafiri wa Reli hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.