Habari za Punde

WAIGIZAJI SASA KUPATA SHAVU KIMATAIFA

''Nataka kuwatengeneza wakina Lupita Nyong'o wengi''
Baada ya kudodora kwa soko la filamu hapa Bongo na Afrika Mashariki kwa ujumla licha ya tasnia hiyo kuajiri vijana wengi lakini imezidi kupoteza mvuto kwa mashabiki wake tofauti na hapo awali.
Kupitia kampuni ya Candy and Candy ya nchini Kenya ambayo ina imefungua tawi lake hapa Bongo kisha kuamua kuandaa kongamano maalum ambalo litahusisha wadau wa filamu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kati lijulikanalo kama 'TAKEU Film Expo' ambalo litafanyika hivi karibuni.
Kongamano hilo ambalo litasaidia kuwakutanisha wadau mbalimbali wa filamu kutoka mataifa husika na wengine kutoka bara la Ulaya kwa ajili ya kutoa semina pia jinsi ya kuboresha filamu hizo kwenda ngazi za kimataifa.
Akizungumzia kongamano hilo mkurugenzi wa kampuni hiyo Joe Kariuki amesema
"Nia yetu ni kuipeleka tasnia ya filamu hapa Bongo na East Africa kwa ujumla kimataifa zaidi ambapo ukitazama hapo awali Bongo movie ilikua juu sana lakini kwasasa inaelekea kupoteza mashabiki,so nipo kwa ajili ya kurudisha hadhi hiyo''

Pia hakusita kutoa wito kwa watu mbalimbali makampuni na mashirika binafsi kushiriki kongamano hilo ili kujifunza na hata kujiajiri wenyewe kupitia ujuzi watakaoupata.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.