Habari za Punde

WAZIRI MHAGAMA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELE MRADI WA NYUMBA ZA CDA DODOMA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista akiwa katika ziara yake kukagua hatua za ukarabati wa nyumba za CDA zilizopo Kikuyu Dodoma kushoto kwake ni Mkurugenzi wa CDA Mhandisi Paskasi Muragili.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mazingira ya nyumba za mradi wa CDA zinazoendelea kukarabatiwa kwa ajili ya watumishi watakao hamia Dodoma awamu zijazo wakati wa ziara yake Kikuyu Dodoma.
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Mhandisi Paskasi Muragili akieleza hatua za ukarabati wa nyumba za Kikuyu kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake tarehe 11 Mei, 2017 Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na Mkurugenzi wa CDA Mhandisi Paskasi Muragili wakati wa ziara yake kukagua maendeleo ya mradi wa nyumba za Kikuyu. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa mradi wa nyumba za Kikuyu unaoendelea Mjini Dodoma. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU- DODOMA
**************************************************
Na. Ripota Wetu, Dodoma
          Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amefanya ziara katika mradi wa nyumba wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma ili kujiridhisha na kazi ya ukarabati inayoendelea. 
Ziara hiyo ilifanyika leo Mei 11, 2017 kwa lengo la kukagua hatua zilizofikiwa na CDA ili kuhakikisha watumishi wa Serikali wanaotarajiwa kuhamia kwa awamu zilizobaki wanaishi kwenye makazi mazuri.
“Tunatarajia ifikapo 28 Juni, mwaka huu CDA iwe imemaliza na kukabidhi nyumba za familia 48 kwa watumishi wa awamu ya pili wanaotarajiwa kuhamia mwezi Julai,”Alisema Waziri Mhagama. 
Aidha, Waziri Mhagama alieleza kuwa nyumba zilizokarabatiwa awamu ya kwanza na ambazo tayari zinakaliwa na watumishi mazingira yake ni mazuri kwani hadi hivi sasa hakuna malalamiko yoyote aliyoyapata kutoka kwa watumishi hao. 
 “Hadi sasa tayari ukarabati umefikia asilimia 80 na sisi kama Serikali tunajukumu la kuisimamia CDA ili kufikia Juni mwaka huu nyumba ziwe zimekabidhiwa zote ili kuwapa mazingira mazuri watumishi wanaotarajiwa kuja awamu mbili zilizobaki”alisisitiza Waziri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu, Mhandisi. Paskasi Muragili alieleza jitihada za ukarabati zinaendelea vizuri na zipo hatua za mwisho na tayari wameandaa mazingira ya kugawa kazi kwa wazabuni zaidi ya mmoja ili kufikia lengo la kumaliza ukarabati kwa wakati.
  “Hadi sasa tunatarajia kupata mzabuni atakaye shughulikia ukarabati wa nyumba 78 za awamu ya tatu na mkataba unatarajiwa kusainiwa mwezi  Juni ili kuendana na kasi ya Serikali ya kufikia adhma yake ya kuhamia Dodoma”.Alisema Mhandisi Muragili.
Waziri Mhagama alimalizia kwa kusisitiza kuwa ukarabati ukamilikie kwa wakati ili ifikapo mwaka 2020 Serikali iwe imehamia Dodoma kwa Awamu zote tatu. 
“Tumeamua,tunatekeleza na tunawahakikishia Watanzania wote ifikapo mwaka 2020 Serikali yote itakuwa imehamia Dodoma”.Alisisitiza Waziri

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.