Habari za Punde

WAKAZI WA MABIBO WANAWISHWA MIGUU BAADA YA KUTOKA KUNUNUA MAHITAJI NDANI YA SOKO LA MABIOBO

 Mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam, Marry Mwakaje, akinawishwa miguu na kijana, Mshua Mjemwa, aliyejiongeza kwa kuanzisha biashara nje ya geti la kutokea ndani ya Soko la Mabibo, ambapo huwanawisha watu kwa Sh. 200 kwa kila mmoja na Sh. 500 kwa aliyevaa viatu vya mvua 'Gambuti' ya mvua na kujipatia kiasi cha Sh. 30,000 hadi 40, 000 kwa siku. Soko hilo kwa sasa limekuwa kero kutokana na kuwa chafu zaidi kwa matope yatokanayo na Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. 
Mdada akinawishwa miguu huku akijiandaa kulipa


 Sehemu ya ndani ya Soko hilo ikiwa imetapakaa tope na kusababish usumbufu kwa wateja wanaofika kujipatia mahitaji.
Chemba ya maji machafu yanayofoka nje ya soko hilo yanayotoka Kiwanda cha Urafiki.
 Mwanamama akinawishwa miguu huku akiwa na mzigo wake kichwani baada ya kutoka kununua ndani ya soko hilo.
Chemba ya maji machafu yanayofoka nje ya soko hilo yanayotoka Kiwanda cha Urafiki.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.