Habari za Punde

WANAFUNZI MAJERUHI WA LUCY VINCENT WAANZA KUZUNGUMZA
Madaktari wa Hospitali ya Mercy, ya Marekani wamesema watoto watatu majeruhi wa ajali ya Lucky Vincent, wanaendelea vyema.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameandika katika ukurasa wake wa faceboook kuwa watoto hao Saidia Ismael, Doreen Mshana na Wilson Tarimo watapelekwa katika makazi maalum ya kuangalia afya zao ikiwa ni pamoja na kupewa mazoezi ya viungo.
Pia watoto hao wameanza kuzungumza na kwa mara ya kwanza mtoto Saidia amesema ‘Helo Tanzania, na Wilson amesema ‘Thank you’.
“Ingawa wataendelea kuwa wodi ya watoto Mercy Hospital kwa sasa hadi madaktari bingwa watakapojiridhisha na hali yao,” ameandika Nyalandu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.