Habari za Punde

WASANII, SHILOLE, MSAGA SUMU NA WENGINEO JUKWAA MOJA JUMAMOSI

WASANII wa muziki wa kizazi kipya na muziki wa Singeli, Msaga Sumu, Dulla Makabila, Shilole, Edu Boy na Pink, Jumamosi Mei 6, watapanda kwenye jukwaa moja katika onesho maalum na Shilawadu, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa JM Manzese Jijini Dar es Salaam. 
Mratibu wa onyesho hilo Soud Brown, alisema kuwa onyesho hilo ambalo ni maalum na la kipekee limepelekwa Mazense kwa lengo la kutoa burudani kwa wakazi wa eneo hilo, waliokosa burudani kama hizo kwa muda mrefu. 
Aidha alisema kuwa wana amini kuwa kila msanii aliyetajwa kushiriki katika onyesho hilo, atakuwa na mambo mapya ya kuwaburudisha mashabiki wake wa pande hizo na kupagawisha kwa burudani ya aina yake kwa wakazi wa mazense, ambao hawajawahi kupata muunganiko wa wasanii kama hao. 

Brown alisema kuwa onyesho hilo linatarajia kuanza majira ya saa 2, usiku kwa kila msanii kutoa burudani kwa muda wa kutosha. 
"Kama mratibu ninaamini kila shabiki wa muziki wa kizazi kipya atakayepata nafasi ya  kuja kwenye onyesho letu atapata burudani ya kutosha kutoka 
kwa kila msanii tuliyemwalika maana wote ni wasanii wazuri na wakali wenye  
nyimbo zinazobamba hivi sasa''. alisema Brown. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.