Habari za Punde

ZIARA YA BULEMBO KITETO

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabaraza ya Jumuia za CCM na Mabalozi wa CCM wa kumi zilizo karibu na Makao Makuu ya  Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara leo katika Ukumbi wa CCM Wilaya hiyo.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, baada ya kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM, Wilayani humo baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya kikazi. (Picha na Bashir Nkoromo)
Mlezi wa CCM, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Mbunge wa Hanang Dk. Mary Nagu akisalimia wajumbe baada ya kutambulishwa katika mkutano wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo, katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Kiteto mkoani huo leo.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara,  Pazo Mwalima akimkaribisha kuzungumza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo, wakati wa kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Mabaraza ya Jumuia za CCM na Mabalozi wa CCM wa kumi zilizo karibu na Makao Makuu ya  Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara leo katika Ukumbi wa CCM Wilaya hiyo.
Wajumbe wakishangilia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo alipozungumza nao katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.