Habari za Punde

ATHUMAN NYAMLANI AJITOA MBIO ZA KUWANIA URAIS TFF

Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani amejitoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
Nyamlani aliwasilisha barua TFF leo Jumapili Juni 25, mwaka huu ikiwa ni siku moja tu tangu Kamati ya Uchaguzi ipitishe jina lake kuwa miongoni mwa wagombea 10 wanaowania nafasi hiyo ya urais. Sababu aliyoeleza ni masuala binafsi.
Kwa msingi huo, wagombea wanaobaki kwenye kinyang’anyiro na kuhitajika kufika kwenye usaili kuanzia Juni 29, mwaka huu ni tisa wakiongozwa na Rais wa sasa, Jamal Malinzi anayetetea nafasi.
Mbali ya Malinzi wengine wanaowania nafasi hiyo ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.
Waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais na kurejesha fomu wako Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.
Mbali ya nafasi za urais na makamu rais, Abdallah Mussa - aliyekuwa akiwania nafasi ya kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji TFF kutoka Kanda Na. 1 (Mikoa ya Kagera na Geita) aliondolewa kwa sababu ya kutoambatanisha kivuli cha cheti ya elimu ya sekondari.
Hivyo wagombea wa nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:

Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;
 1. Soloum Chama
 2. Kaliro Samson
 3. Leopold Mukebezi

Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;
 1. Vedastus Lufano
 2. Ephraim Majinge
 3. Samwel Daniel
 4. Aaron Nyanda

Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;
 1. Benista Rugora
 2. Mbasha Matutu
 3. Stanslaus Nyongo

Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;
 1. Omari Walii
 2. Sarah Chao
 3. Peter Temu

Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;
 1. John Kadutu
 2. Issa Bukuku
 3. Abubakar Zebo
 4. Francis Michael

Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;
 1. Kenneth Pesambili
 2. Baraka Mazengo

Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa;
 1. Elias Mwanjala
 2. Cyprian Kuyava
 3. Erick Ambakisye
 4. Abousuphyan Silliah

Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;
 1. James Mhagama
 2. Golden Sanga
 3. Vicent Majili
 4. Yono Kevela

Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;
 1. Athuman Kambi
 2. Dunstan Mkundi

Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida; 
 1. Hussein Mwamba
 2. Mohamed Aden
 3. Musa Sima
 4. Stewart Masima 
 5. Ally Suru
 6. George Benedict

Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;
 1. Charles Mwakambaya
 2. Gabriel Makwawe
 3. Francis Ndulane
 4. Hassan Othman ‘Hassanol’ 

Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga
 1. Khalid Mohamed
 2. Goodluck Moshi
 3. Thabit Kandoro

Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam
 1. Emmanuel Ashery
 2. Ayoub Nyenzi
 3. Saleh Alawi
 4. Shaffih Dauda
 5. Abdul Sauko
 6. Peter Mhinzi
 7. Ally Kamtande
 8. Said Tully
 9. Mussa Kisoky
 10. Lameck Nyambaya
 11. Ramadhani Nassib
 12. Aziz Khalfan
 13. Jamhuri Kihwelo
 14. Saad Kawemba
 15. Bakari Malima

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.