Habari za Punde

BALOZI WILSON MASILINGI MGENI RASMI FUTARI YA PAMOJA DMV

Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Col. Aldoph Mutta (kushoto) akimlaki Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi siku ya Jumamosi June 17, 2017 siku Mhe. Balozi alipokua mgeni rasmi kwenye futari ya pamoja inayoandaliwa na Jumuiya ya Waislam DMV (TAMCO) Silver Spring, Maryland.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akipokewa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislam DMV (TAMCO) ustaadh Ally Mohamed mara tu alipowasili na kujumuika na wanajumuiya hao waislam wa DMV na marafiki zao katika futari ya pamoja iliyofanyika siku ya Jumamosi June 17, 2017 Silver Spring, Maryland.
Mwenyekiti wa TAMCO ustaadh Ally Mohamed akimwongoza Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi ndani ya ukumbi.
Kutoka (kushoto) ni Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Col. Aldoph Mutta, mkuu wa idhaa ya Kiswahili Voice of America (VOA) Dr. Hmza Mwamoyo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi na The Maryland House of Delegates Legislative District 41 Baltimore City Mhe. Bilal Ali ambaye nae alialikwa na Jumuiya hiyo kwenye futari ya pamoja DMV. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi na The Maryland House of Delegates Legislative District 41 Baltimore City Mhe. Bilal Ali wakiongozwa na mkuu wa idhaa ya Kiswahili Voice of America (VOA) Dr. Hmza Mwamoyo kwenye futari ya pamoja iliyofanyika siku ya Jumamosi June 17, 2017 Silver Spring, Maryland.
Kutoka (kushoto) ni Mke wa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico mama Marystela Masilingi, Balozi Liberata Mulamula, Zawadi Sakapala na dada Jasmine wakipata futari.
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja,

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.