Habari za Punde

BULEMBO AANZA ZIARA MKOANI GEITA, LEO APIGA MIKUTANO WILAYANI BUKOMBE
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo na msafara wake, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM na Jumuia zake mkoa wa Kagera, wakati wakiagana tayari kuingia katika mkoa wa Geita leo asubuhi.

Alhaj Abdallah Bulembo akiagana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera.

Mwandishi wa Star Tv Abdallah Tilata aliyeko kwenye msafara wa Alhaj Abulembo akiagana na Katibu Tawala wa Halmashari ya Wilaya ya Muleba Benjamin Mwikasyele kabla ya mafara kwenda mkoani Geita. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Mwandishi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo Happines Mtweve akiagana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera.

Ben Mugisha ambaye ni Dereva wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Bulembo, akiagana na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Rahel Ndengeleka.

Baadhi ya Waandishi wa Habari walioko kwenye msafara wa Alhaj Bulembo wakiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa Chama na Jumuia mkoa wa Kagera
RASMI MKOANI GEITA🔽

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM na Jumuia zake waliompokea katika eneo la Nampalahala baada ya kuingia katika mkoa huo kuendelea na ziara yake ya Kichama, leo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipeana mkono wa furaha na Katibu wa CCM mkoa wa GeitaAdam Ngalawa wakati wa mapokezi hayo.

Baadhi ya waliopo katika msafara wa Alhaj Bulembo wakipata kifungua kinywa katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, kabla ya kikao kuanza leo. Kushoto ni Victoria Patrick na Happines Mtweve na kulia ni Ben Mugisha.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akivishwa vazi la heshima la Kabila la Wasukuma alipowasili wilayani Bukombe, leo. Anayemvisha ni Mzee wa Bukombe, Hakim Mstaafu Joseph Bulugu.

Alhaj Abdallah Bulembo akishukuru baada ya kupewa heshima hiyo.

Alhaj Bulembo akiwasili ukubini kuongoza kikao cha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za Chama, Mabalozi na watendaji wa Serikali.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akijadili jambo na Mbunge wa Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Geita Doto Biteko wakati wa kikao hicho.

Ofisa wa Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Omari Kalolo akisalimia wakati wa kikao hicho.

Ofisa kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Fadhili Mlami akisalimia wakati wa kikao hicho.

Katibu wa Siasa na Oganaizesheni Daniel Mgaya akisalimia wakati wa kikao hicho.

Wajumbe ukumbini wakati wa kikao hicho.

Katibu wa CCM mkoa wa Geita Adam Ngalawa akizungumza wakati wa kikao hicho.

Wajumbe ukumbini

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Bukombe Jacob Butachange, akisalimia baada ya kutambulishwa katika kikao hicho.

Mbunge wa Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Geita Doto Biteko akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho. Kushoto ni Alhaj Bulembo na Kulia ni Butachage

Mjumbe w Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Bukombe, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za Chama, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, leo. PICHA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.