Habari za Punde

DC KASESELA AKESHA MGODINI NYAKAVANGALA KUOKOA MAITI YA MCHIMBAJI

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika mgodi wa nyakavangala uliopo katika Kata ya malengamakali Mkoani Iringa wakati wa Juhudi za kuuokoa mwili wa marehemu viskadi nyenza katika shimo alilosimama Mkuu huyo wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akisaiadiana na wachimbaji madini katika mgodi wa nyakavangala ili kuokoa mwili wa marehemu Nyenza.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipokuwa akiwasili katika mgodi wa nyakavangala uliopo Kata ya malengamakali Mkoani Iringa.
**********************************************
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alilazimika kufanya kazi ya uokoaji wa maiti ya mchimbaji madini katika mgodi wa Nyakavangala bwana Vaspa nyenza mkazi wa Itengulinyi Kata ya Ifunda wilaya ya Iringa kwa takribani masaa kumi na nane.
Kasesela alisema kuwa alianza kazi hiyo majira ya saa mbili asubuhi alipowasili katika mgodi huyo wa Nyakavangala lakini yeye,waandishi wa habari na viongozi wengine wa wilaya ya Iringa walijitahidi kuokoa mwili wa marehemu hadi majira ya saa sita usiku lakini zoezi hilo lilikuwa likiendelea.
"Hadi saizi tumepiga dua zote lakini hali ngumu sijui nini kinaendelea katika hili shimo maana waokoaji kila wakiukaribia mwili wa marehemu miamba laini inavungika na kujaza udongo ndani ya shimo ndio maana mmeniona naangaika na ndugu wa marehemu kujaribu kusali huku na kule lakini hali ni ngumu hadi muda huu wa saa tano usiku"alisema Kasesela.
Aidha Kasesela aliwataka ndugu wa marehemu na viongozi mbalimbali kuwa na subila wakati wanalishugulikia swala la kuokoa mwili wa mpendwa wao kwa kuwa wameshaukaria mahali ulipo.
"Ungalia tayari kichwa na kiwiliwili vimeshaonekana kwa hiyo tumebakiza sehemu ndogo tu naombeni tuwe wavumilivu kwa kuwa tuvumilia toka siku ya jumapili hadi usiku huu basi tuungane kumuombea mwenzetu ili tutoe mwili wake ukiwa salama" alisema Kasesela.
Haya yamemkuta mchimbaji mwenzenu hivyo nawataka kuwa makini wakati wa uchimbaji wa madini katika mgodi huu wa nyakavangala la sivyo mgodi huu utafungwa sio muda.
Lakini mwili wa Vaspa Nyenza umepatikana saa 7 na dakika 50 usiku na msafara kuelekea mortuary umeanza na Mazishi kufanyika Kijiji cha Itengulinyi Ifunda kesho asubuhi kuanzia saa 3 au 4 hivi.
Kwa upande wake Chief inspector Mayunga Ngele aliwataka wachimbaji wote kutochimba tena kwenye mashimo yaliyozuiliwa ili kuepusha ajali mbalimbali hapo mgodini kwa kuwa hata huyo marehemu na wenzake walishakatwa kuchimba katika shimo hilo ambalo lilikuwa kwenye hali mbaya ya kuanguka.
"Tamaa ndio zimemponza huyu marehemu maana tuliwakataza lakini mwenyewe waliingia kinyemela kwa lengo la kwenda kuchimba kwa wizi kwenye shimo lilokataliwa ndio maana yamewakuta hayo kama wangekuwa wameusikia ushauri wetu basi tusingefika hapa tulipo usiku huu "alisema inspector Ngele.
Naye Thomas masuka mmiliki wa mgodi wa Nyakavangala alimshukuru mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa jitihada zake za kuhakikisha kila kitu kianda kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na serikali na kuahidi kuwa gharama za kuuokoa mwili hadi kuufikisha kwako ni kwake na ndugu hawatalipia pesa yoyote ile.
"Kuanzia kutokea kwa kifo chake,uokoaji na kuusafirisha mwili wa marehemu huyu gharama zote nitazilipa mimi kama mmiliki wa mgodi huu kwa mujibu wa sheria za madini hata angekuwa Mwananchi wa kigoma,Mwanza, Mbeya, Bukoba na sehemu yoyote ile ndani ya Tanzania basi ni wajibu wangu kuhakikisha mwili wa marehemu unafika mali pake kwa usalama unaotakiwa" alisema Masuka.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.