Habari za Punde

DIRISHA LA USAJILI WA WACHEZAJI MSIMU WA LIGI KUU 2017/2018 KUFUNGULIWA JUNI 15

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatangaza kufungua dirisha la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa mashindano wa 2017/2018.
Dirisha hilo linafunguliwa Juni 15, mwaka huu na litafungwa Agosti 6, mwaka huu hivyo kila timu inayoshiriki michuano tajawa hapo juu, inaarifiwa kufuata kalenda hiyo ambayo tunaitangaza sasa.
Tahadhali, hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa timu ambazo hazitakamilisha usajili kama ilivyotokea msimu uliopita kwa baadhi ya timu kushindwa kufanya kusajili kwa wakati na dirisha likafungwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.