Habari za Punde

EVERTON KUVAA 'JEZI' YA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA DHIDI YAO NA MAN U LIGI YA ENGLAND

 Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa, Abbas Tarimba (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza ujio wa Timu ya Everton inayotarajia kuwasili nchini Julai 12 mwaka huu ambapo itacheza mchezo wa kiafiki na timu ya Gor Mahia ya Kenya Julai 13 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika jana kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro. Kulia ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Meena, (kushoto) ni Kaimu Mkurgenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Michezo, ALex Mkeyenge (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mku wa Kampuni ya SportPesa,Pavel Slavkov.
 Abbas akionyesha Kitabu cha Everton kinachoiongelea Tanzania

**********************************
UJIO wa timu ya soka ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya England, unatarajiwa kutangaza na kukuza utalii wa Tanzania.
Everton wanatarajiwa kutua nchini Julai 12 kwa ajili ya mchezo maalum dhidi ya mabingwa wa SportPesa, Gor Mahia.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 13 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tanzania, Abbas Tarimba, alisema kuwa ujio wa Everton nchini utasaidia kukuza utalii.
Alisema kuwa timu hiyo inatarajia kuja nchini ikiwa na baadhi ya nyota wake kwa ajili ya mchezo maalum ambapo pia watatembelea katika vivutio mbalimbali.
Tarimba alisema kuwa wameanza kufanya taratibu katika mechi za Ligi Kuu ya England msimu ujao, ambapo Everton itavaa jezi zenye nembo ya vivutio vinavyopatikana Tanzania ili kutangaza zaidi utalii.
Aidha alisema kuwa wachezaji hao watakapofika nchini na kuona vivutio mbalimbali, wataenda kusimulia nchini kwao na baadaye Tanzania itapata wageni wengi kutoka nje.
“Tunatarajia kwamba Everton watatumia fursa hii kuutangaza utalii wa Tanzania kwani baada ya kurejea kwao na kuhadithia yale waliyoyaona, itakuwa rahisi kuwashawishi watalii wengi zaidi kuja kutembelea vivutio.
“Pia tunatarajia kuweka taratibu kwamba wataporudi kwenye Ligi ya England, watavaa jezi zenye nembo ya vivutio vya Tanzania ili kutangaza utalii zaidi,” alisema Tarimba.
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii, Geofrey Meena, alisema kuwa watatumia vyema sekta ya michezo kuhakikisha inakuwa na manufaa hasa kwa ujio wa timu ya Everton.
Alisema kuwa kupitia ziara hiyo, kipato katika sekta mbalimbali kitaongezeka na kukuza pato la taifa.

 Abbas (kushoto) akijadiliana jambo na Pavel Slavkov, wakati wa mkutano huo
 Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF, Salum Madadi, akizungumza wakati wa mkutano huo.
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Meena, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.