Habari za Punde

IDARA YA SERA NA MIPANGO OFISI YA WAZIRI MKUU YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUIMARISHA TAARIFA ZA HALI YA HEWA NA MIFUMO YA TAHADHARI TANGA, KILIMANJARO NA ARUSHA

Mhandisi wa mitambo ya kusoma Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka 
ya Hali ya Hewa Bw. Michael Minja akieleza matumizi ya kifaa cha 
kupima mvua kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walipotembelea 
vituo hivyo vinavyotekelezwa na Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya 
Hewa na Mifumo ya Tahadhari uliopo Lushoto Mkoani Tanga Juni 6, 2017.
Mhasibu Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Consolata Mazigo akiuliza 
swali kwa Mhandisi wa mitambo ya hali ya hewa Bw. Michael Minja wakati 
wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya 
Hewa na Mifumo ya Tahadhari wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 6, 2017 
Lushoto Tanga.
Mhandisi wa mitambo ya kusoma Taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka
ya Hali ya Hewa Bw. Michael Minja akieleza matumizi ya mtambo wa 
kisasa wa usomaji wa taarifa za hali ya hewa kwa Maafisa kutoka Ofisi 
ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa 
mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari
ulio chini ya Ofisi hiyo. KWA PICHA ZAIDI BOFUA HAPA
Baadhi ya Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakinukuu maelezo ya Fundi  
Sanifu Mkuu Bonde la Pangani Bw. Vendelin Basso (hayupo pichani)  
wakati wa mkutano wa kutathimini Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha
 Taarifa  za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari katika Ukumbi wa 
mikutano wa Ofisi hiyo Kilimanjaro, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi 
Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. 
Grace Moshi Juni 7, 2017.
Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Mto Pangani Bw. Vendelin Basso akiwasilisha
utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo 
ya Tahadhari kwa upande wa Bonde la Mto Pangani mkoani Kilimanjaro 
wakati wa ukaguzi wa Utekelezaji wa mradi huo uliofanywa na Ofisi ya 
Waziri Mkuu Juni 7, 2017.
Mratibu Taifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo
ya Tahadhari Bw.Daniel Alfei akiwasilisha mada yake wakati wa mkutano 
wa kutathimini Utekelezaji wa mradi huo kwa upande wa Bonde la Mto 
Pangani Mkoani Kilimanjaro Juni 7, 2017.
Fundi Sanifu Hydrojia kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Bw.Paul Damian  
akimuonesha Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya 
Waziri Mkuu Bi. Grace Moshi kifaa cha kusafirisha taarifa za 
kuongezeka au kupungua kwa maji mtoni (Intelligent Top Cap) wakati wa 
tathimini ya utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya 
Hewa na Mifumo ya Tahadhari Juni 7, 2017 Mkoani Kilimanjaro.
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiangalia namna ya Kifaa cha 
kupima joto Ardhi (Themometer) ikiwa ni moja ya kifaa kilichofungwa 
katika Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na 
Mifumo ya Tahadhari eneo la Lyamungu Wilayani Hai.
Msaidizi wa masuala ya Hali ya Hewa Bw. Mbaraka Shaghira (katikati) 
akieleza matumizi ya Kifaa cha kupima upepo kwa Maafisa kutoka Ofisi 
ya Waziri Mkuu walipotembelea Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya 
Hewa na Mifumo ya Tahadhari ili kuona Utekelezaji wake eneo la Kituo 
cha Tafiti cha Lyamungu Wilayani Hai.
Fundi Sanifu Mkuu Bonde la mto Pangani Bw. Vendelin Basso kionesha 
namna ya kusoma kifaa cha kupima kina cha maji kwa Mchumi Idara ya 
Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Bivelyne Muchumbuzi kilichopo 
katika Mto Malala wakati wa ukaguzi wa Utekelezaji wa mradi wa 
Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari chini ya 
Ofisi hiyo Juni 7, 2017. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.