Habari za Punde

JE WAJUA?? WALICHOKIFANYA SIMBA KWA NIYONZIMA WALISHAKIFANYA KWA ATHUMANI CHINA

IKIWA imepita zaidi ya miaka ishirini na tatu ( 23) baada ya Simba sports club imerudia kufanya ilichokifanya mwaka 1994 baada ya kufanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji mwenye akili nyingi awapo dimbani Haruna Niyonzima 
Mwaka 1994 Simba ilimsajili mchezaji wa nafasi ya kiungo mshambuliaji Athumani Abdallah China (mchezaji aliyekuwa anapendwa mno na wanayanga wakiamini ni damu yao) 
Athumani Abdallah China aliichezea Yanga kwa mafanikio makubwa lakini mwishoni mwa msimu wa mwaka 1991 aliomba kwenda zake nje kutafuta nafasi ya kucheza soka la kulipwa enzi hizo kwa ahadi atakaporejea atajiunga tena kwenye kikosi cha timu hiyo kama wataona bado ana uwezo wa kuitumikia Yanga sports club.
Kinyume na matarajio yao wana Yanga wengi wakiongozwa na mfadhili wao marehemu Abbas Gulamali...... China alipoamua kurudi nchini hakurudi tena Yanga akaamua kujiunga na Simba sports club watani wa jadi wa Yanga... kabla ya CHINA kusajiliwa Simba wachezaji THOMAS KIPESE na GODWIN ASWILE walitangulia kujiunga na Simba mwaka 1993 lakini wanayanga wengi hawakuumizwa na usajili huu kwa vile waliamini hao hawakuwa wachezaji walioziteka nyoyo zao.
Kwa kugundua hilo la Yanga kutoumizwa na usajili wa KIPESE na ASWILE kwenda Simba mfadhili wa simba AZIM DEWJI alijipanga kuhakikisha ATHUMANI CHINA anatua Simba kwa gharama yeyote ile pindi alipopota habari ya kurejea kwake nchini kiungo mshambuliaji huyo mrefu mwembamba ( yellow man ).
AZIM DEWJI alifanya hivi baada ya Yanga kuwasajili wachezaji vipenzi vya wanasimba method mogella na Hamisi Gaga mwaka 1992 kabla ya kumsainisha zamoyoni mogella mwaka 1993.
Hakika usajili wa Athumani Abdallah China Simba mwaka 1994 ulikuja kufunika usajili wa kina mogella kwenda Yanga si kwa sababu kina mogella hawakuwa wachezaji wazuri hapana kilichowaumiza yanga ni kitendo cha mchezaji waliyeamini wamemkuza wenyewe na kumtengenezea jina kuamua kucheza simba wakati wao bado wanamtaka hili lilikuwa shambulizi moja lililojibu mashambulizi matatu ya yanga ndani ya miaka miwili...GULAMALI alipambana sana kuhakikisha Athumani AbdallahChina anasaini Yanga lakini juhudi zake zilikwama kwani AZIM DEWJI alijipanga kama ambavyo Mohammed Dewji alijipanga kwa usajili huu wa HARUNA ABIZIMANA FADHILI NIYONZIMA.
Kwangu mimi tokea usajili wa Athumani Abdallah China Simba haikuwahi kusajili mchezaji yeyote wa Yanga aliyewaumiza wanayanga kutokana na ubora wake mpaka alivyonaswa Haruna Niyonzima msimu huu 

WATOTO WA MJINI WANASEMA SIMBA WAMEIBIWA DEMU, WAO WAMEIBA MKE

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.