Habari za Punde

KAMERA YA MAFOTO BLOG MITAANI LEO, VIROBA VIPYA SASA 'CHUPANI'

Kamera ya Mafoto Blog, imefumania picha za chupa zinazobeba pombe zilizopigwa marufuku maarufu kama Viroba, ambavyo kwa sasa badala ya kuwa katika pakiti zinakuwa ndani ya Chupa hizi, ambazo mpaka sasa sina uhakika kama tayari vifungashio hivi vimepitishwa na TBS kwa kukizi vigezo.

Hata hivyo kwa vifungashio hivi kwa upeo wa kamera ya Mafoto Blog, bado si suluhisho la kumaliza tatizo la ulevi holela kwa vijana kutokana na jinsi kifungashio kilivyo, ambapo sidhani hata kama kitahalalishwa na TBS kitauzwa zaidi ya sh. 5000 na kumfanya kijana kujipanga kikamilifu kupata kumudu kukitumia na kwa wakati husika.

Na iwapo kitauzwa kwa bei ile ile iliyokuwa ya Viroba vya Plastiki bado tatizo la ulevi kwa vijana litazidi mara dufu ya lilivyokuwa kwani wataamini kuwa sasa wanatumia kihalali baada ya kuwa katika vifungashio vipya. Yangu ni hayo tu.......

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.