Habari za Punde

MADRID WALIVYOWAFANYA KITU MBAYA VIBIBI KIZEE VYA TURIN JUVE JANA USIKUMshambuliaji wa RealMadrid akiruka juu kupiga Tik Tak ikiaminiwa ni kumlipa mfungaji wa bao la Juventus, 

Mandzukic
, aliyefunga balo lake kwa stail hiyo. Katika mchezo huo wa Fainali ya UEFA Champions Ship, Madrid walishinda mabao 4-1 na kutwaa tena kombe hilo.

JANA Usiku katika fainali ya michuano ya UEFA timu ya Real Madrid, ilifanikiwa kutetea taji lake la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Juventus ya Italia mchezo uliopigwa Uwanja wa Millennium mjini Cardiff, Wales.
Alikuwa ni Cristiano Ronaldo, Mwanasoka Bora Duniani, aliefungua pazia la mabao ya Real Madrid kwa kuifungia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya
 20 akimalizia pasi ya Daniel Carvajal – lakini bao hilo halikudumu, kwani Mandzukic aliisawazishia Juve dakika saba baadaye kwa tik tak akimalizia mpira wa Gonzalo Higuain.

Ronaldo alipiga mabao mawili moja kila kipindi, huku maba

o mengine yakifungwa na Casemiro na Marco Asensio na la Juve limefungwa na Mario Mandzukic kukamilisha msimu wa Ligi ya Mabingwa 2017.
Hilo linakuwa taji la 12 la michuano hiyo kwa Real Madrid tangu ikiitwa Klabu Bingwa Ulaya, baada ya awali kulitwaa katika miaka ya 1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002, 2014 na 2016.
Real Madrid wakishangilia na taji lao baada ya kukabidhiwa Uwanja wa Millennium mjini Cardiff , jana usiku
****************************************************
Na hiyo ndiyo klabu iliyotwaa mara nyingi zaidi taji hilo, ikifuatiwa na AC Milan ya Italia mara saba, Bayern Munich ya Ujerumani, Barcelona ya Hispania na Liverpool ya England zote mara tano kila moja.
Timu hizo zikaenda kupumzika zikiwa zimefungana 1-1 na wakati kikitarajiwa kipindi kigumu cha pili, mambo yakawa mepesi kwa kocha Mfaransa mwenye asili yaq Algeria, Zinadine ZIdane baada ya timu yake kufanikiwa kuongeza mabao matatu.
Alianza Casemiro dakika ya 61 kabla ya Ronaldo kufunga la tatu dakika ya 64 na Marco Asensio kumaliza kazi kwa bao la nne dakika ya 90.
Juve ilimaliza pungufu, baada ya mshambuliaji wake, Juan Cuadrado aliyetokea benchi dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Andrea Barzagli kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 84 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, kufuatia kumsukuma beki wa Real, Sergio Ramos.
Mabao mawili ya leo yanamfanya Ronaldo aendelee kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa, akifikisha mabao 105 tangu 2003 alipoanza kucheza michuano hiyo akiwa Manchester United ya England. Na anafuatiwa na hasimu wake mkubwa, Muargentina Lionel Messi mwenye mabao 94 tangu mwaka 2005 akiwa na Barcelona. 
Akipiga bao lake la pili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.