Habari za Punde

MASHABIKI ELFU 10 WA SOKA WA JIJI LA NAIROBI KUTUA DAR KATIKA FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP KESHO

MASHABIKI wa Soka kutona jiji la Nairobi kuhamia Dar es salaam kesho kushuhudia miamba ya soka wa nchini Kenya wenye upinzani wa jadi, Gor Mahia na AFC Leopards, zitapokutana katika uwanja wa Uhuru kwenye fainali ya SportPesa Super Cup.
Si mara ya kwanza kwa miamba hii ya soka nchini Kenya kukutana  katika fainali ardhi ya ugenini.
Ikumbukwe mnamo mwaka 1980 katika michuano ya CECAFA ( sasa Kagame Cup) nchini Malawi walikutana katika fainali baada ya Gor Mahia kuwapiga 4-2 wenyeji Limbe kwenye mikwaju ya penati. 
AFC Leopards ambao wakati huo walikuwa wakijulikana kwa jina la Abaluhya FC waliitandika timu ya jeshi la Zambia Green Buffaloes 1-0.
Katika fainali hiyo Gor Mahia walishinda 3-2 dakika za jioni kabisa baada ya matokeo ya sare ya 2-2 kudumu mpaka dakika ya 85 .
Ni moja ya fainali za kukumbukwa sana za wababe hawa wa soka nchini Kenya walipokutana nje ya Kenya kwa mara ya kwanza na Gor Mahia kunyakua kombe la CECAFA kwa mara ya kwanza.
SportPesa wanastahili pongezi za dhati kuyaleta mashindano haya Tanzania na kuwapa burudani ya aina yake wadau wa soka Afrika mashariki .
Tayari taarifa za awali zimetanabaisha mashabiki takribani 10,000 toka Kenya wanaingia kesho jijini Dar es salaam kuushuhudia mtanange huu wa kihistori.
Upinzani wa jadi kati ya Gor Mahia na AFC Leopards unajulikana kama ‘ mashemeji ‘ Derby ikiwa mechi namba nne kwa mvuto zaidi Afrika . Ya kwanza ni Al Ahly vs Zamaleki , Kaiser Chiefs vs Orlando Pirates na ya tatu ni Yanga SC vs Simba SC .

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.