Habari za Punde

MASHINE ZA KIELETRONIKI KUANZA KUTUMIA MAGOGONI DAR

Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Serikali inatarajia  kutoa huduma za ukatishaji wa tiketi kwa njia ya mfumo wa kielekroniki katika kivuko cha Magogoni ili kudhibiti mapato yanayopotea kiholela.
Akiongea na Maelezo Jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Dkt. Musa Mgwatu alisema kukamilika kwa mfumo huo utakaogharimu bilioni 1.1 kutasaidia kuiongezea mapato serikali kwani mfumo huo utafanyakazi kwa njia za kielekroniki.
“Ujenzi wa mashine za kielektroniki umeshaanza na kukamilika kwa upande wa magogoni, Mkandarasi anatarajia kuanza ufungaji wa mashine hizo upande wa Kigamboni wiki hii,” alifafanua Dkt. Mgwatu.
Dkt. Mgwatu alisema Mkandarasi wa mradi huo anatarajia kukamilisha uwekaji wa mashine hizo julai 25 mwaka huu na utumiaji wa mashine hizo utaanza kutumika tu mara baada ya makabidhiano kutoka kwa mkandarasi.  
Akizungumzia gharama za kuvuka Dkt. Mgwatu amesema, gharama za kuvuka zitabaki pale pale na hakutakuwa na ongezeko lolote mashine hizo zitakapoanza kutumika.
Bwana Ismail Juma, mkazi wa Kigamboni amesema kuanzishwa kwa mfumo huo kumekuja wakati muafaka na kutasaidia kuiongezea mapato serikali na kuepusha upotevu wa mapato katika vivuko hivyo.
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  aliwaagiza TEMESA kufunga mfumo kamili wa kupokea nauli wa elektroniki ambao utadhibiti ukwepaji wa kulipa nauli ili kuongeza mapato.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.