Habari za Punde

MUFTI WA TANZANIA AWASILI MKOANI KILIMANJARO KWA SWALA YA EID EL FITRI

Mufti wa Tanzania Sheik Aboubakary Zubeiry Ali akiwasili katika mmoja wa misikiti iliyopo wilayani Hai kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi.
Mufti wa Tanzania,Sheakh Aboubakary Zubeiry Ali akifungua kitambaa katika kuweka jiwe la Msingi kuashiria kuendelea kwa ujenzi wa jengo hilo litakalotumika kama Madrasa.
*************************************
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubery Ali amesema kwamba mwenye mamlaka ya kutangaza mwezi ni ya Mufti Mkuu baada ya kushauriana na Kamati ya Mwezi. Baada ya Mufti kujiridhisha ndipo Bakwata huutangazia Umma kuhusu kuandama kwa mwezi. 
Hivyo basi Mufti wa Tanzania amesema jana mjini Moshi kwamba leo Jumamosi Juni 24, 2017 kamati ya mwezi itaendelea kufuatilia kuandama kwa mwezi na ikiwa utaandama watautangazia umma kuwa Jumapili itakua Eid El Fitr na ikiwa hautoonekana basi itabidi kukamilisha siku 30 za mfungo wa Ramadhan na Eid kuswaliwa Jumatatu In Shaa Allah.
Baadhi ya wanawake wa Dini ya Kiislamu walipofika kwa ajili ya kumpokea Mufti wa Tanzania,Sheikh Aboubakary Zubery Ali.
Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheakh Aboubakary Zubeiry Ali akiwa na waliompokea katika lango la kutokea eneo la watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alipowasili jana mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Swala ya Idd El- Fitr inayotaraji kufanika kitaifa mkoani humo. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akitia aini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kilimajaro (KIA).
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akiteta jambo na Shekh Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Gari maalumu kwa ajili ya Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali 
Msafara wa Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali ukitoka katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) .
Gwaride la vijana katika kumpokea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali 
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akiwa na viongozi pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wanawake wa Dini ya Kiislamu walipofika kwa ajili ya kumpokea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali 
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akiwasili katika mmoja wa miskiti iliyopo wilayani Hai kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi. 
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akifungua kitambaa katika jiwe la Msini kuashiria kuendelea kwa ujenzi wa jengo hilo litakalotumika kama Madrasa.
Mapokezi mwakubwa kwa Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali.
Jengo la Ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai ambalo Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali amefika kwa ajili ya uzinduzi wake.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akisalimiana na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili katika ofisi za Bakwata wilaya ya Hai ka ajili ya ufunguzi wake.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akisalimiana na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili katika ofisi za Bakwata wilaya ya Hai ka ajili ya ufunguzi wake.
Furaha ya kutembelewa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akizindua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kufungua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akiondoka baada ya kufungua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika msikiti wa Masjid Shafii kwa ajili ya uzinduzi.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akikata utepe kuuzindua rasmi Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Aliakizindua rasmi Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Katibu wa Bakwata wilaya ya Hai,Mwl Mohamed Mbowe akisoma risala mbele ya Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali wakati wa uzinduzi rasmi wa msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akipokea risala hiyo
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akizungumza mara baada ya kuzindua Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai.
Na Dixon Busagaga, Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.