Habari za Punde

NJEMBA YADAKWA IKITAKA KUINGIZA SIMU GEREZA LA AHABUSU KEKO JIJINI DAR

Jeshi la Magereza jana Jumapili limemkamata kijana mmoja aitwaye Ramadhani Nombo akiwa na simu tano alizozificha kwenye mapande ya nyama aliyokuwa ameletea ndugu zake walio mahabusu katika gereza la mahabusu la Keko jijini Dar e salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za jeshi hilo, hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.
“Kutokana na umakini wa askari wetu mara alipofika na kuomba kuwaone ndugu zake walio mahabusu na kuwapa chakula walibaini kwamba ndani yake kuna simu” imesema taarifa hiyo. Haikutajwa nyama na hizo simu alikuwa anapalekewa mahabusu gani hapo gerezani.
Taarifa zinasema kimsingi kijana huyo amevunja Kifungu cha 86 (1) cha Sheria ya Magereza sura ya 56 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 ambayo inakataza mtu yeyote kuingiza magerezani kitu chochote kisichoruhusiwa.
Kifungu hicho kinatamka bayana kwamba endapo ikithibitika mtu yeyote amekamatwa na kuingiza kitu chochote ambacho hakiruhusiwi kuingizwa gerezani, atahukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita (6) gerezani au faini au vyote kwa pamoja.
Mtuhumiwa Ramadhani Nombo akiwa amebeba mapande ya nyama ambayo yanatuhumiwa kuwa na simu tano ndani yake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.