Habari za Punde

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI WA RUVU JUU MLANDIZI MKOANI PWANI PIA AZINDUA VIWANDA VINGINE MKOANI HUMO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Balozi wa India hapa Nchini Sandeep Arya, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa wa Pwani na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ruvu Juu Mlandizi Mkoani Pwani.
Sehemu ya Mradi huo wa maji wa Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Mfuko wa sandarusi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo kabla ya kuzindua kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilijaribu Trekta mojawapo katika kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine akifungua kiwanda hicho cha nondo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.