Habari za Punde

SIMBA YAMNASA ALLY SHOMARY WA MTIBWA SUGAR

SIMBA imesajili beki Ally Shomary kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuimarisha kikosi kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.
Shomary anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa ambapo alitambulishwa rasmi  na Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na kukabidhiwa jezi ya klabu hiyo.
Makamu wa rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amekiri kusajiliwa kwa mchezaji huyo na kusema wanaendelea na usajili ili kuimarisha timu yao ambayo mwakani itakuwa inakabiliwa na mashindano ya kimataifa.
Shomary anaungana na kipa Emanuel Elias Mseja, mabeki Jamal Mwambeleko waliosajiliwa kutoka Mbao FC, Yussuf Mlipili kutoka Toto Africans zote za Mwanza, Shomary Kapombe na mshambuliaji John Bocco kutoka Azam FC. 
Pia na kipa Aishi Manula, ambaye na wakwa mbioni kumrejesha mshambuliaji wao wa zamani Mganda Emmanuel Okwi kutoka SC Villa ya Uganda.
Na mshambuliaji wa FC Nkana ya Zambia, Walter Bwalya ambaye pia ni miongoni mwa wachezaji waliotajwa kuwa kwenye mpango wa Simba.
Simba inafanya usajili wa kishindo, baada ya kufanikiwa kukata tiketi ya michuano ya Afrika mwakani baada ya kutofanikiwa kushiriki kwa miaka mitano mfululizo.
Simba itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani kufuatia kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mwaka huu kwa kuifunga Mbao FC mabao 2-1 katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.