Habari za Punde

SINGIDA UTD YAFUNGASHIWA VILAGO NA AFC LEOPARDS KATIKA MICHUANO YA SPORTPESA SUPER CUP

 Mshambuliaji wa Singida Utd, Nhivi Simbarashe (wa pili kulia) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa AFC Leopards, Joshua Mawira, (kulia) wakati wa mchezo wa fungua dimba mashindano ya SportPesa Super Cup, yaliyoanza leo kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) ni  Marcus Abwao.  Katika mchezo huo uliomalizika hivi punde AFC Leopard wameibuka kidedea kwa ushindi wa penati 5-4 baada ya kumalizika dakika 90 zikiwa sare ya 1-1. Mchezo unaofuata hivi punde ni Yanga vs Tusker
 Wachezaji wa AFC Leopards, wapigwa na butwaa baada ya kufungwa bao katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza.
Mchezaji wa Singida United, Mtasa Wisdom, akiruka kuokoa katikati ya wachezaji wa AFC Leopards.
 Hatari langoni mwa AFC Leopards
Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakiwa jukwaani wakifuatilia mchezo huo kabla ya wao kukipiga na Tusker katika mchezo wa pili

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.