Habari za Punde

SIWEZI KUIBEZA MICHUANO YA SPORTPESA SUPER CUP: LWANDAMINA

KOCHA Mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Yanga, George Lwandamina amesema hawezi kuidharau michuano ya SportPesa SuperCup ambayo itaweza kumpatia taswira ya kikosi chake msimu ujao.
Yanga ni miongoni mwa timu ambazo zitashiriki michuano ya SportPesa ambayo inatarajia kuanza keshokutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Mashindano ya SportPesa Super Cup yanashirikisha timu nane, Nne kutoka Tanzania na Nne kutoka Kenya.
Mbali na Yanga timu nyingine ambazo zitashiriki michuani hiyo ni Simba, Singida United na Jang’ombe Boys kwa Tanzania wakati Kenya kuna AFC Leopard, Nakulu All Stars, Tusker FC na Gor Mahia.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kocha Lwandimina alisema amejipanga vizuri na maandalizi ya michuano hiyo na kwamba atahakikisha anaipa uzito mkubwa michuano hiyo kutokana kwani yatamsaidia kufahamu makosa kuelekea katika kufanya usajili msimu huu.
Alisema wanajua ni moja ya fursa muhimu kwa timu yake endapo itaweza kubeba ubingwa huo na kupata nafasi ya kucheza na klabu kubwa barani Ulaya kama Everton.
“Si michuano ya kubeza kiasi hicho, lazima tuipe uzito na tubebe ubingwa huu, kwanza itatutapatia morali ya kikosi chetu na kufahamu udhaifu wetu.
“Tunaenda kucheza na timu za nje, zina wachezaji wazuri lazima tutapata kitu toka kwao kufahamu udhaifu wetu ili tusije kufanya makossa katika usajili,”alisema.

Bingwa wa michuano ya atacheza na klabu ya Everton ya England, mchezo ambao utakung’utwa Julai 13, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.