Habari za Punde

SPIKA NDUGAI APOKEA VITABU KUTOKA KWA MTANDAO WA KUONDOA UMASKINI KWA AJILI YA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISINI KWAKE MJINI DODOMA LEO

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea vitabu kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa kuondoa umasikini, Ndg. Mungwe Athman (katikati) kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tukio lililofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, wa pili kushoto ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa na Wageni wengine ni Wajumbe wa tume ya Utumishi wa Bunge wakiongozwa na Mhe. Mussa Zungu (nyuma kulia)
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na  Mwenyekiti wa Mtandao wa kuondoa umasikini, Ndg. Mungwe Athman (kushoto)kabla ya Makabidhiano ya vitabu kwa Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , tukio lililofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akionyesha moja ya kitabu alichokabidhiwa na Mtandao wa kuondoa umasikini, vitabu walivyokabidhi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athman na kulia ni Mjumbe wa tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Peter Msigwa, nyuma yake pia ni Wajumbe wa tume ya utumishi wa Bunge ambao ni Mhe. Mussa Zungu na Mhe. Mary Chatanda. Picha na Ofisi ya Bunge

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.