Habari za Punde

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAWAPIMA AFYA VIONGOZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaelezea wafanyakazi wa   Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara japo mara moja kwa mwaka wakati wafanyakazi hao walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.

 Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Hesabu  kutoka  Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Fatuma Chillo akiuliza ni muda gani mzuri wa  kupima shinikizo la   damu mwilini (BP) wakati wafanyakazi wa shirika hilo walipofika katika  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya upimaji wa afya zao. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Katibu wa  NHC  Martin Mdoe.
Mkurugenzi wa Ukaguzi  wa Hesabu kutoka  Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Fatuma Chillo akichukuliwa kipimo cha damu na Alex Onesmo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo Moyo, figo na kisukari. Viongozi wa NHC walifika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
  Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akimpima urefu na uzito  Mkurugenzi   wa   Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Mwanza Benedict Kilimba  wakati viongozi wa Taasisi hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akimpima shinikizo la damu  (BP)  Meneja  Uendeleza Miliki wa   Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Haikamen Mlekio  wakati viongozi wa Taasisi hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoa wa Tabora Dickson Ngonde  akichukuliwa kipimo cha damu na Alex Onesmo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo Moyo, figo, tezi dume  na kisukari. Viongozi wa NHC walifika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
 Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akimpima shinikizo la damu  (BP)  Meneja  Oparesheni za Mikoa  wa   Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Maneno Mahenge   wakati viongozi wa Shirika hilo walipofika JKCI  leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao.
 Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Peter Issack akichukuliwa kipimo cha damu na Alex Onesmo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo Moyo, figo, tezi dume  na kisukari. Viongozi wa NHC walifika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya upimaji wa afya zao. Picha na JKCI

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.