Habari za Punde

TANZIA: SHABIKI MAARUFU WA YANGA 'ALLY YANGA' AFARIKI DUNIA

 Gari alilokuwa amepanda Ally Yanga na wenzake katika msafara wa Mbio za Mwenge baada ya kupata ajali hiyo.

SHABIKI maarufu wa Klabu ya Yanga, Ally Yanga, amefariki dunia hii leo kwa ajali ya gari akiwa na wenzake katika msafara wa Mbio za Mwenge huko maeneo ya Mpwapwa.

Hizi ni Habari zilizothibithishwa na kutolewa na Kitengo cha Habari cha Yanga
Uongozi wa Yanaga SC umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha shabiki wao, Ally Yanga, hakika MUNGU ni mwema , faraja ya MUNGU wetu ikawe kwa familia katika kipindi chote cha majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao, Pia nasi Yanga kifo chake kina acha pengo kubwa kwa nafasi yake ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa na alikuwa balozi mzuri kama mwanachama na shabiki mkubwa  wa timu yetu, Bwana alitoa, Bwana ametwaa.

Imetolewa na Idara ya Habarai na mawasiliano.
Young Africans Sports Club.
20-6-2017.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.