Habari za Punde

TFF YAIGOMEA BMT YAPANGA KUENDELEA NA MCHAKATO WA UCHAGUZI KAMA KAWAIDA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema halitasitisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu licha ya kupokea barua ya zuio kutoka Baraza la Michezo Tanzania (BMT).
Akizungumza na wandishi wa habari leo mchana kwenye Ofisi za TFF, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine (pichani kuli) alikiri kupokea barua ya BMT na kusema wamewaandikia barua ya kutaka kukutana nao mapema.
“Tunatarajia kukutana nao maana namini wanafanya hivi kwa sababu ya afya ya mpira wa miguu lakini hatutasimamisha uchaguzi kwa sababu utakuwa nje ya katiba,” alisema Selestine.
Aidha Selestine alisema katiba ya TFF inawakata kufanya uchaguzi kabla ya Agosti kumalizika hivyo wakisitisha mchakato huo watakuwa wanakiuka katiba.
“Uchaguzi Mkuu wa TFF ni agenda moja tu katika mkutano huo hivyo ukisitisha mchakato wa uchaguzi unaweza kujikuta umefika mwakani bila uchaguzi kufanyika,  pia kamati inayosimamia uchaguzi ipo kihalali kulingana na katiba ya TFF,” alisema Selestine.
Juni 13 Baraza la Michezo lilimwandikia barua Katibu Mkuu wa TFF kutaka kusitishwa kwa uchaguzi wa viongozi wakuu wa TFF kwa sababu halijajulishwa kuwepo kwa uchaguzi huo.
Pia barua hiyo iliwataarifu TFF kuwa kamati ya nidhamu, rufaa na usuluhishi ya Baraza inataka kukutana na kamati ya utendaji ya TFF Julai Mosi saa nne asubuhi katika ofisi za Baraza zilizopo Uwanja wa Taifa.
Lakini pia Selestine alisema wao wana katiba yao inayojitegemea na wanapaswa kuwasilisha BMT matokeo ya uchaguzi na  siyo kuwajulisha juu ya mchakato wa uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.