Habari za Punde

'YANGA NI KIMYA KIMYA' AJIBU AKAMILISHA DEAL SASA KUVAA UZI WA KIJANI NA NJANO JANGWANI

Kiungo mchezaji wa Simba, Ibrahim Ajib, amemalizana na Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili hii leo ambapo sasa atavaa uzi wa Kijani na Njano kwa Wanajangwani hao kwa  msimu ujao.
Ajib baada ya kutisha kwa misimu kadhaa akiwa na wekundu hao wa mtaa wa Msimbazi. Vuta nikuvute ya fundi huyo wa mpira na viongozi wake imechukuwa ni ya muda mrefu lakini mwisho wa siku vigogo hao wakakubali kushindwa kimya kimya na kumwachia kutimkia Jangwani.
Ibrahim Ajibu, amepewa pesa ya usajili Sh Milioni 50 pamoja na gari ndogo ya kutembelea huku usajili huo ukifanywa kwa siri kubwa ili kukwepa ‘msala’ walioupata baada ya kumsajili beki wa kulia Hassan Ramadhan ‘Kessy’ akiwa hajamaliza mkataba wake msimu uliopita.
Mkataba wa Ajibu na Simba utamalizika mapema mwezi ujao na viongozi wa Yanga wamepanga kuweka hadharani kila kitu wakati huo huku sasa wakipambana kukanusha kila kitu kuhusiana na uhamisho huo.
Huu unakuwa usajili wa pili kwa Yanga baada ya jana kumalizana na beki wa kati wa Taifa Jang’ombe Abdallah Hajji.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.