Habari za Punde

YANGA SC, AZAM FC WANAVYOHAHA KUMNASA MBARAKA YUSUPH, NANI KURAMBA DUME?

WAKATI vyombo vya habari nchini vikiripoti habari za Mshambuliaji wa Kagera Suga, Mbaraka Yusuph, kujiunga na Yanga huku Vinongozi wa Klabu hiyo pia wakieleza kutokuwa na wasiwasi na mchezaji huyo kujiunga na Klabu nyingine, tayari mchezaji huyo ameonekana akikabidhiwa Jezi ya Timu ya Azam Fc, hiyo kimaanisha tayari amesaini mkataba na timu hiyo.
Yanga walikaririwa na Gazeti moja na michezo lililomkalili mmoja wa viongozi wa Klab hiyo, akisema kuwa wana uhakika na wa kunasa saini ya mshambuliaji huyo ambaye amepewa baraka na Klabu yake ya Kagera Sugar kujiunga na Yanga.
Pamoja na Mbaraka kuonekana katika baadhi ya mitandao ya kijamii akikabidhiwa jezi ya Azam lakini bado 'eti' habari za kuaminika kutoka Yanga zinasema kuwa 'eti' Mchezaji huyo tayari alikwishamalizana na Klabu yao ya Yanga, huku pia viongozi wa klabu yake ya zamani ya Kagera Sugar wakiamini mambo yanaendelea vizuri kwa mchezaji wao kujiunga na Yanga inayotarajia kushiriki michuano ya Kimataifa mwakani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.