Habari za Punde

ZIARA YA MWANAMUZIKI FERRE GOLA, CHRISTIAN BELLA SHULE YA UHURU MCHANGANYIKO

 Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo, Ferre Gola, (wa pili kulia) Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Ltd, Teddy Mapunda (kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru mchanganyiko, Anna Mshana, kwa pamoja wakipaka rangi katika ukuta wa chumba cha darasa la Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, wakati walipofika shuleni hapo kwa ajili ya kujionea mazingira ya shule hiyo, baada ya kuomba kusaidiwa mahitaji hayo, ambapo msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo, Ferre Gola, (kushoto) na Christian Bella,  kwa pamoja wakipaka rangi katika ukuta wa chumba cha darasa la Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, wakati walipofika shuleni hapo kwa ajili ya kujionea mazingira ya shule hiyo, baada ya kuomba kusaidiwa mahitaji hayo, ambapo msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
********************************************
Mwanamuziki nyota wa Kidemokrasia ya Congo, Fere Gora na mwanamuziki nyota nchini, Christian Bella watafanya onyesho pamoja kwenye ukumbi wa King Solomon Jumamosi.
Onyesho hilo limepangwa kuanza Saa 2.00 usiku, ni maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru wa nchi ya DR Congo.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Montage Tanzania Limited, Teddy Mapunda alisema kuwa maandalizi ya onyesho hilo yamekamilika na kuwaomba wadau kufika kwa wingi ili kupata radha tofauti ya Fere Gora na Christian Bella.
Teddy amesema kuwa awali waliamua kufanya onyesho moja tu la VIP kwenye ukumbi wa Serena Hotel, lakini kutokana na kutambua mashabiki mbalimbali wa Fere Gora wa hapa nchini, wameamua kuongeza onyesho hilo maalum pia.
Hii ni mara ya kwanza kwa mwanamDR Congo kufanya onyesho Tanzania. Mashabiki watarajie kupata radha mbalimbali za nyimbo maarufu kama Vita Imana, 100 kilos na nyingine kibao.
Akizungumzia ujio wake nchini, Fere amesema kuwa ni fursa kwake kufanya onyesho Tanzania na kuahidi kufanya kile ambacho mashabiki wanakitarajia.
“Nimekuja hapa kufanya onyesho na kutoa burudani kwa mashabiki wangu, nimejiandaa vilivyo na naamini pia Bella atafanya kama mimi,” alisema Fere.
Wanamuziki hao jana walishiriki katika zoezi maalum la kung'arisha madarasa ya shule ya Uhuru mchanganyiko kama sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Uhuru.
Kwa mujibu wa Mapunda mbali ya kufanya zoezi la kupaka rangi, pia wameadhimia kutoa misaada mbalimbali kama Tv kubwa, deki, jiko la gesi na mtungi, vifaa vya michezo, jezi seti 3 mipira na madawati.
Amesema kuwa msaada mwingine utakwenda kwa shule Wama Nakayama, iliyopo Nyamisati ambayo itapewa madawati na misaada mbalimbali.
 Mwanamuzki wa Kimataifa kutoka nchini Congo, Ferre Gola (kulia) akisaini katika moja ya picha ya kujifunzia iliyobandikwa kwenye Chumba ca darasa katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko, baada ya kumaliza kupaka rangi katika chumba hicho, walipofika kukabidhi ndoo za rangi ikiwa ni msaada uliotokana na mauzo ya Meza za onyesho maalumu la mwanamuzki huyo. Kushoto ni Mwanamuziki Christiani Bella. 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Ltd, Teddy Mapunda, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mwanamuziki wa kimataifa kutoka Congo, Ferre Gola (wa pili kulia) na Christian Bella (kulia) walipofika SHule ya Uhuru Mchanganyiko kwa ajili ya kukabidhi na kupaka rangi katika baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule hiyo. msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mwanamuziki wa kimataifa kutoka Congo, Ferre Gola (wa pili kulia) na Christian Bella (kulia) walipofika Shule ya Uhuru Mchanganyiko kwa ajili ya kukabidhi na kupaka rangi katika baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule hiyo. msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwanamuziki Christian Bella, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mwanamuziki wa kimataifa kutoka Congo, Ferre Gola (wa pili kulia) na Christian Bella (kulia) walipofika Shule ya Uhuru Mchanganyiko kwa ajili ya kukabidhi na kupaka rangi katika baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule hiyo. msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Wakitembelea maeneo ya shule hiyo.....
 Ferre Gola, akisaini katika kitabu cha wageni
Christiani Bella, akisaini katika kitabu cha wageni....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.