Habari za Punde

BALOZI IDDI ATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA DAR ES SALAAM

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa  Dara es salaam, Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Slum Ali na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Nd. Felix Lyaniva.
Balozi Seif akikagua Bidhaa katika Banda la Shirika la Miga Chaa Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiangalia Vyombo vya kupikia katika banda la 
Wafanyabiara kutoka Nchini Misri.
Balozi Seif akitoka nje ya baada ya kuangalia Banda la Bidhaa za Wafanyabiashara, Taasisi na Wajasiriamali wa 
Zanzibar.
Balozi Seif Kulia na Waziri wa Biashara na Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali wakiangalia bidhaa mbali mbali za khanga na vitenge vilivyotengenezwa na Tanzania Textile Lilited.
***************************************************
Makamu wa ili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza
Wazalishaji wa bidhaa za Viungo kujitahidi kuongeza nguvu za
uzalishaji wa Kilimo cha Viungo ili kuirejeshea hadhi yake Tanzania ya
kuongoza katika uzalishaji wa Bidhaa hizo Duniani.
Alisema wazalishaji hao ni vyema wakazingatia pia ushauri na maelekezo
ya Wataalamu pamoja na Viongozi katika kuona Kilimo cha mazao ya
Viungo kinaimarika na kuleta tija.
Balozi Seif AlI Iddi alitoa agizo hilo mara baada ya kuyatembelea
mabanda mbali mbali ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar
es salaam yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Uendelezaji Biashara Tanzania
{Tan Trade} kwenye Viwanja vya Julius Nyerere Bara bara ya Kilwa
Jijini Dar es salaam.
Tarehe 10 Julai 2107 ni siku maalum ya Bidha mbali mbali za Viungo
kwenye Maonyesho hayo {Spice Day } yanayotembelewa na zaidi ya
Wananchi na Wageni wapatao Laki Moja kwa Siku.
Balozi Seif alisema yapo masoko mengi Duniani hasa Nchi zilizoko
katika ukanda wa Bara ya Asia yanayohitaji kufanya Biashara za bidhaa
zinazotokana na Viungo jambo ambalo wazalishaji hao wanaweza kuitumia
fursa hiyo katika kuongeza kipato.
Alisema kwa vile bidhaa za Viungo zitaendelea kuwa muhimu katika
Maisha ya Bianaadamu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zitashirikiana katika kuona maonyesho
ya bidhaa tofauti yanayokuwa yakifanyika kwa pande zote mbili
yanafanikiwa.
Makamu wa Pili wa Frais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Mamlaka ya
Uendelezaji Biashara Tanzania { Tan Trade } pamoja na Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji Tanzania Bara kwa uamuzi wao wa kutenga
siku maalum kwa bidhaa maalum ndani ya Maonyesho hayo ya 41 ya
Biashara Dar es salaam.
Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam ya Mwaka huu
yamefana sana kutokana na utaratibu mzuri wa bidhaa kutengewa siku
Maalum ”. Alisema Balozi Seif.
Mapema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara ya
Kimataifa ya Dar es salaam { Tan Trade } Nd. Edwin Rutageruka
alisema Nchi 30 Duniani zilizojumuisha Makampuni 515 na yale ya
Wazalendo yapatayo 2,520 yameshiriki kwenye Maonyesho hayo ya
Kimataifa Dar es salaam.
Nd. Rutageruka alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba
Mikataba ipatayo Milioni 2,000,000 inatarajiwa kusainiwa mara baada ya
kumalizika kwa maonyesho hayo ya Kinmataifa .
Alisema zaidi ya wananchi na Wageni mbali mbali wapatao Laki 100,000
hutembelea mabanda mbali mbali kwa siku kujionea na kujipatia huduma
kulingana na mahitaji yao.
Akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuzungumza na wadau
mbali mbali wa Maonyesho hayo Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko
Zanzibar Balozi Amina Salum Ali alisema Tanzania ilikuwa na sifa kubwa
ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na Viungo Duniani.
Alisema sifa hiyo inapaswa kuchukuliwa juhudi za ziada kwa pande zote
mbili za Tanzania Bara na Zanzibar ili iweze kuongoza tena hasa
kipindi hichi kinachoelekea katika Tanzania ya Viwanda.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika ziara hiyo ya
Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam alitembelea
mabanda ya Wafanyabiashara kutoka Nchini Misri, Idara ya Mpiga Chapa
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Banda la Shimono la Singapore
pamoja na lile la shirika la Taifa la Biashara Zanzibar {ZSTC}.
Mengine ni Z.H. Group, Mahanjumati, Kamisheni ya Utalii Zanzibar,
Zaindan Chukwani Zanzibar, Jiko la Shamba Ndijani, Banda la Viwanda
Vidogo vidogo {SIDO}, Bagharesa Group,Metl, Mfuko wa Fursa sawa kwa
wote, Jeshi la Kujenga Taifa {JKT}, Wizaya ya Viwanda Biashara na
Uwekezaji pamoja na Banda la Bidhaa za Viungo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.