Habari za Punde

DC ALI HAPI ANOGESHA MTANANGE WA MABALOZI vs PROPERTY INTERNATIONAL KUADHIMISHA MIAKA 55 YA UHURU WA ALGERIA, AKABIDHI KOMBE

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, akimkabidhi Kikombe Nahodha wa timu ya Property International, Saleh, baada ya timu hiyo kuibuka washindi katika mchezo wa kirafiki kati yao na Mabalozi wanaoziwakilisha timu zao nchini, uliokuwa maalumu kwa ajili ya kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Algeria, uliochezwa kwenye Uwanja wa JK Yourth Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Property walishinda mabao 2-1. Katikati ni Balozi wa Algeria nchini, Saad Bal Abed.
 Mshambuliaji wa Property, Salum Careca, akijiandaa kupiga shuti huku akizongwa na mchezaji wa Mabalozi, Ibrahim Salim.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najim, akichuana kuwania mpira na Saleh.
 Saleh, akichanja mbuga.
 Idrisa Nassor (kushoto) akiwatoka mabeki wa Mabalozi....
 Idrisa Nassor, akichuana kuwania mpira na kipa wa Mabalozi. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

 Kikosi cha timu ya Mabalozi
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, akimkabidhi Kikombe Nahodha wa timu ya Property International, Saleh, baada ya timu hiyo kuibuka washindi katika mchezo wa kirafiki kati yao na Mabalozi wanaoziwakilisha timu zao nchini, uliokuwa maalumu kwa ajili ya kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Algeria, uliochezwa kwenye Uwanja wa JK Yourth Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Property walishinda mabao 2-1. (katikati yao) ni Balozi wa Algeria nchini, Saad Bal Abed. Kulia aliyekaa ni Balozi wa Parestina nchini, Hazim Shabat.
 Nahodha wa Property, Saleh, akimkabidhi kikombe hicho Balozi wa Algeria kwa heshima, baada ya kukabidhiwa. 

 DC Hapi, akizungumza na wachezaji (hawapo pichani) baada ya kumalizika kwa mtanange huo.
 Furaha ya ushindi
 Picha ya pamoja wachezaji wa timu zote mbili na mgeni rasmi,
Kikosi cha timu ya Property International.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.