Habari za Punde

DC HAPI AIAGIZA POLISI KUMKAMATA NA KUMTIA NDANI MASAA 48 MBUNGE HALIMA MDEE

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi ameliagiza jeshi la Polisi Kinondoni kumkamata Mbunge wa Kawe Halima Mdee kwa kosa la kutoa kauli za matusi, dhihaka na uchochezi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi kwa ujumla.
Hapi ameagiza mbunge huyo kukamatwa, kukaa korokoroni kwa saa 48, kuhojiwa na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kwa maneno aliyoyatoa jana akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema mtaa wa ufipa. 
Hapi amesema kuwa maneno aliyoyatoa Mdee ni matusi yenye lengo la kuleta uchochezi unaoweza kuhatarisha amani na utulivu.
"Sitamvumilia mwanasiasa yeyote atakayethubutu kutoa kauli za matusi dhidi ya Mh. Rais, au zenye kutaka kuleta uchochezi katika wilaya yangu."
Alisema DC Hapi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.