Habari za Punde

DHAMANA YA MALINZI NA WASAIDIZI WAKE YAGONGA MWAMBA, WARUDISHWA RUMANDE HADI JULAI 17


Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
VIGOGO wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Rais Jamal Malinzi, Katibu wake, Selestine Mwesigwa na Mhasibu, Nsiande Isawafo, wamerudishwa rumande hadi Julai 17,  hadi upepelezi wa kesi yao utakapokamilika.
Malinzi na wenzake leo  tena walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya kupelekwa rumande Julai 29, kufuatia kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika benki ya Stanbic, Dar es Salaam.

Wiki iliyopita Hakimu mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbord Mashauri aliwanyima dhamana baada ya mabishano ya kisheria baina ya mawakili wa utetezi dhidi ya mawakili wa Serikali na kuwapangia kuja mahakaman kwa mara ya pili hii leo.
Hata hivyo, hali imeendeelea kuwa mbaya upande wa Malinzi na wenzake baada ya leo pia kunyimwa dhamana na kurudishwa rumande. 
Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake Nsiande Isawafo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.