Habari za Punde

KAMISHNA WA BIMA DKT. SAQWARE ATEMBELEA MAONESHO YA 41 YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR

Kamishna ya Mamlaka ya Buima Tanzania, (TIRA), Dkt. Abdallah Baghayo Saqware, (mwenye suti), akipatiwa maelezo ya kiutendaji kutoka kwa Afisa Masoko na Mauzo wa Wakala wa Huduma za Ununuzi za Serikali, (GPSA), Bw.David Isaya, (kulia), wakati Kamishna huyo alipotembelea banda la Wakala huyo wa Serikali kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye vwianja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ambako maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanaendelea. Wakwanza kushoto ni Afsia Masoko na Utafiti wa Mamlaka ya Bima Tanzania, Bw.Augustino Nicholaus.
Dkt. Saqware (kulia), akiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa TIRA, Bi. Adelarde Muganyizi, (wapili kulia), walipotembeela banda la GPSA. Kushoto ni Bw.Isaya.
Dkt. Saqware, pia alitembeela banda la Mfuko wa Pensehni wa PPF, ambako aliomba kupatiwa huduma ya kupata taarifa za michango ayke yeye kama mwanachama, ambapo baada ya sekunde chache alikabidhiwa taarifa yake ya michango. Kushoto ni Afisa Mtafiti wa PPF, Bi.Elaine Maro. 
Kamishna ya Bima nchini, Dkt. Abdallah Baghayo Saqware, (kulia), na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa TIRA, Bi. Adelarde Muganyizi, (wapili kulia), wakipatiwa maelezo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. A bdul Njaidi walipotembeela banda la Mfuko huo leo Julai 10, 2017.
Dkt. Saqware akipewa mfuko wenye taarifa mbalimbali za PPF naAfisa Mtafiti wa PPF, Bi.Elaine Maro. 
Maafiwa wa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini, kutoka kulia, Bw.David Isaya, amabye ni Afisa Masoko na Mauzo, Bi.Valeri Zambi, Mhasibu, na Bw.Peter Mayila, Afisa Masoko na Mauzo, wakiwa kwenye banda la Wakala huyo wa serikali tayari kuhudumia wananchi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.