Habari za Punde

KIKAO CHA WAZI CHA KUTOA MAONI DHAMIRA YA SERIKALI KUPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI NCHINI

TANGAZO 
Mwaka jana Serikali ilitangaza dhamira ya kupiga marufuku ya kuzalisha, kuuza, kusambaza, uingizaji na matumizi ya mifuko ya plastiki ya kubebea bidhaa nchini kutokana na uchafuzi wa mazingira. Kwa kuwa hatua hiyo ni kubwa, Serikali imeamua kuwashirikisha wadau na wananchi ili kupata maoni yao. Kwahiyo, wananchi wote wanaotaka kutoa maoni kuhusiana na hatua hiyo wanakaribishwa katika mkutano wa wazi wa kupokea maoni utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 22 mwezi Julai 2017 kuanzia saa tatu asubuhi katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na utahudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Mhe. January Makamba (MB). Karibuni wote mtoe maoni na sauti yenu isikike.

Imetolewa na
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Makamu wa Rais, 
S.L.P. 5380,
11406 Dar es Salaam.
Barua Pepe: km@vpo.go.tz
Tovuti: www.vpo.go

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.