Habari za Punde

KWAYA KIBAO KUSINDIKIZA UZINDUZI WA DVD YA ANIONGOZA LEO

KWAYA kutoka madhebu mbalimbali ya kikristo  leo (jumapili) zinatarajia  kushiriki kikamilifu katika tamasha la uzinduzi wa  albamu ya video ya mwimbaji wa muziki wa injili Raymond Mdemu.
Uzinduzi huo utapambwa na tamasha kubwa la uimbaji  litakalofanyika katika viwanja vya Kanisa la Sabato, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es salaam, jana, Mdemu alisema  siku hiyo atazindua DVD  yake yenye nyimbo 10 inayoibatiza jina la Uniongoze.
Alitaja nyimbo zinazopatikana katika albamu hiyo kuwa ni Baba yetu uliyembinguni, Nitaonana na Yesu, Mwokozi  yu mwema, Majaribu ya nisonga, kila saa, Mpe moyo wako, Aniongoza, Ninahaja nawe, Peleka neno,Nifikapo mbiinguni.
“Sisi tuna sema shughuli hii ni kuweka wakfu na kuzindua albamu hii na hakutakuwa na kiingilio kwa wote.Hivyo mwananchi yoyote anakaribishwa kuhudhuria tamasha hili kubwa,”alisema Mdemu maarufu kama Ticha.
Alitaja kwaya zitakazo sindikiza uzinduzi huo kuwa ni kwaya za madhehebu ya kisabato ambazo ni Ilala, Ubungo, Familia ya Injili Yombo, MBagala, Keko, Temeke, Mabalozi na Vijana SDA Temeke.
“Pia tumealika kwaya za dhebu la Anglikana  ambazo ni Mtakatifu  Bathlomayo Ubungo, Mtakatifu  Thomaso Yombo, Watakatifu wote na Mtakatifu Albano Posta,”alisema Ticha.
Alisema kwaya zingine zitakazopamba uzinduzi huo wa aina yake ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambazo ni kutoka Usharika wa Kipawa, Buza, Segerea, Yombo na Makangarawe.
“Pia kutakuwa na vikundi vingi na waimbaji binafsi.Shughuli itaa saa 3:00 asubuhi hadi jioni.Kanisa liko Temeke mkabala na kituo cha polisi Chang’ombe.Njooni tumwimbie Mungu,”alisema.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.