Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA BANDA LA PROPERTY INTERNATIONAL, MAONYESHO YA SABASABA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem, kuhusu Ndege ya Kampuni hiyo inayopiga picha za juu kwa muda mfupi wakati wa upimaji wa Viwanja (Unmanned Ariel Vehcle As 1200)  wakati Makamu wa Rais alipotembelea Banda la Maonyesho la Kampui hiyo kwenye Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.  Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye Banda hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem.
Maelezo yakiendelea.
Ziara ndani ya Banda hilo ikiendelea.....
Makamu wa Rais akionyeshwa ramani za viwanja vinavyouzwa na Kampuni hiyo.
Makamu wa Rais akionyeshwa picha za juu zinazopigwa na ndege zisizo na rubani katika Screen iliyopo ndani ya Banda hilo.
Maelezo yakiendelea....
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Teknolojia ya 'Mega Panel' wa Kampuni ya Property International, Jonathana Kibona, wakati alipotembelea Banda la maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa la Kampuni hiyo ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo. 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akishika moja kati ya Panel zinazotumika kujengea kuta ili kuthibitisha maelezo aliyopewa kuhusu ubora wa kuta zinazojengwa na Panel hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem, akiendelea kutoa maelezo kwa Makamu wa Rais kuhusu ujenzi wa nyumba zinazojengwa na Kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kuuza na kukopesha Viwanja.
 Muonekano wa nje ya Banda hilo
 Mmoja kati ya wateja akihudumiwa.


 Wananchi wakiendelea kuonyeshwa ramani za Viwanja.
 Wafanyakazi wa Property wakipiga kazi ndani ya Banda.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.