Habari za Punde

MAKONDA: KAMPUNI YA PROPERTY INTERNATIONAL INASAIDIA KUONDOA TATIZO LA MIGOGOLO YA ARDHI JIJINI DAR ES SALAAM


Na Mwandishi Wetu, Dar
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema miongoni mwa Makampuni Binafsi yanayoisaidia Serikali kwa kufanya kazi ya uuzaji na upimaji wa Viwanja vya Viwanda na Makazi, ni Kampuni ya Property International ambayo ni miongoni mwa makampuni ambayo yanafanya vizuri na  kama mkuu wa mkoa bado hajapata malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu migogolo ya ardhi.
Akizungumza katika Kipindi cha Sema Kweli kinachorushwa kila Ijumaa na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, alisema kuwa, amekuwa akipata malalamiko kadhaa kutoka kwa wananchi juu ya migogolo hiyo inayotokana na kuuziwa ama kupimiwa viwanja na makampuni ambayo hayajajitosheleza katika kufanya kazi hiyo baada ya kuidhinishwa na Serikali.
Aidha alisema kuwa kutokana na suala hilo kumekuwa na ugumu wa Serikali kukusanya mapato 'Kodi ya majengo' kutokana na wananchi kujijengea makazi holela bila kupata vibali vya ujenzi, baada ya kuuziana maeneo kienyeji bila kupimwa na kupatiwa hati, jambo ambalo kwa sasa linafanyiwa kazi kwa kasi na baadhi ya makampuni binafsi ikiwamo ya Property International, yanayoshirikiana na Selikali katika kifanya kazi hiyo.
Makonda alimpongeza Waziri William Lukuvi, kwa kazi ngumu anayofanya ikiwa ni pamoja na ya ulasimishaji wa makazi ili kwenda na viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya kuzitambua nyumba na kuzipa madaraja tofauti kurahisisha upatikanaji wa kodi ya majengo, na mpangilio wa miji unaotakiwa huku Serikali ikiendelea kuwakaribisha wapimaji biasfi ili kuendana na kasi.
''Wapimaji binafsi watasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa Watumishi na Vifaa vya kisasa vinavyorahisisha upimaji wa haraka na kwa wakati, lakini Manispaa zinatakiwa kuwapa ushirikiano makampuni hayo kwa kuwapa na kuwatambua ili Serikali inapotoa Hati isitokee mgongano kutokana na maeneo husika kupimwa na watu watatu tofauti''. alisema
Akiongelea kuhusu Makampuni binafsi yanayotambulika na kuisaidia Serikali kufanya kazi ya Upimaji, aliitaja Kampuni ya Property International, ambayo ina jumla ya Viwanja 240 vya Viwanda huko eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambapo anayehitaji Heka hata 500 hadi 1000 anaweza kupata ambavyo tayari vimepimwa na zaidi ya Viwanja 800 vya Makazi na Biashara vilivyopimwa katika mradi huo.
Akizungumza na Mtandao huu, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Property International, Haleem Zahran , alisema kuwa Kampuni imefarijika sana 
baada ya kusikia taarifa za serikali kutambua mchango na juhudi zinazofanywa na kampuni yake katika kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha suala la kupanga na kupima Viwanja katika maeneo mbalimbali ili wananchi kuweza kupata makazi yaliyo salama.
Hata hivyo alimpongeza Mkuu wa Mkoa Paul Makonda na Waziri Lukuvi kwa kazi kubwa wanavyofanya katika Sekta hiyo ili kuendana na kasi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo baada ya muda kila mwananchi atakuwa akiishi katika eneo linalotambulika na kupunguza migogolo ya ardhi.
‘’Kama kampuni bado tuna  mikakati mikubwa ya kuendelea kuongeza mashine za kisasa za kurahisisha upimaji wa maeneo kwa haraka na uhakika''. Alisema Haleem
Aidha alisema kuwa Kampuni yake inaendelea na juhudi za kuiunga mkono Serikali na kwamba haitalewa sifa kwa kutambulika huko bali itaongeza jitihada na kupambana ili kuhakikisha inaisadia Serikali kupanga na kupima maeneo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.