Habari za Punde

MALINZI, AVEVA NGOMA BADO NGUMU, KESI YAHAIRISHWA


UPELELEZI wa kesi inayomkabili Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal 
Malinzi na wenzake, haujakamilika.


Malinzi na wenzake ambao wanasota mahabusu 
kwenye Gereza la Keko, walipanda kizimbani jana 
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati shauri linalowakabili lilipopelekwa kwa kutajwa.

Washitakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa 
Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande 
Mwanga ambao wakikabiliwa na mashitaka 28, 
ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za M
arekani, 375,418.


Malinzi na wenzake walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbrad Mashauri ambapo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, alidai shauri lilipelekwa kwa kutajwa na kwamba upelelezi haujakamilika na kuomba kuahirishwa hadi tarehe nyingine.
Washitakiwa hao walikuwa wakiwakilishwa na mawakili James Bwana
na Abraham Senguji hawakuwa na pingamizi na 
kuhusu kuahirishwa kwa shauri hilo.
Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 
11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa walirudishwa mahabusu.
Baadhi ya mashitaka yanayowakabili washitakiwa hao, Malinzi na Selestine wanadaiwa Juni 5, mwaka jana, m
aeneo ya jiji la Dar es Salaam, 
walighushi nyaraka ya maazimio ya kamati tendaji ya 
Juni 5, mwaka jana kwa lengo la kuonesha kuwa 
kamati hiyo ya TFF imelenga kubadili mtia saini wa 
shirikisho hilo katika akaunti za benki kutoka Edgar 
Masoud kwenda kwa Mwanga.
Selestine anadaiwa Septemba Mosi, mwaka jana, katika 
benki ya Stanbic iliyopo Kinondoni, Dar es Salaam, 
alitoa nyaraka hizo zilizoghushiwa Juni 5, 
mwaka jana, kuonesha kuwa TFF imebadilisha mtia
saini wa akaunti zake za benki kutoka Masoud
kwenda kwa Mwanda kitu ambacho alijua si kweli.
Washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa Septemba Mosi na Oktoba 19m mwaka
jana maeneo ya jiji hilo, walitakatisha fedha ambazo 
ni Dola za Marekani 375,418 huku wakijua kwamba 
fedha hizo ni zao la kughushi.
Malinzi na Selestine wanadaiwa kati ya 
Septemba Mosi na Oktoba 19, mwaka jana, maeneo 
ya Benki ya Stanbic Kinondoni, walighushi Dola za 
Marekani 375,418.
Mwanga anadaiwa kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19,mwaka jana,
katika ofisi za TFF, aliwasadia Malinzi na 
Selestine kuchukua fedha hizo kutoka Benki ya
Stanbic huku akijua kwamba fedha hizo zimetokana 
na kughushiwa kwa fomu ya kuchukulia fedha ya
Machi 15, mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.