Habari za Punde

MBUNGE WA KAWE HALIMA MDEE ALIPOFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMTUKANA RAIS

Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Halima mdee akisalimiana na Mbunge wa Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mhe Esther Bulaya, akiwa amehifadhiwa katika ukumbi wa Wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa kesi yake.
Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Halima mdee, akiwa amehifadhiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salam leo akisubiri kusomewa kesi yake.
Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Halima mdee, akiwa amehifadhiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salam leo akisubiri kusomewa kesi yake.
************************************************
*****************************************************
Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chadema, Halima amepandishwa katika kizimbani cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kumtukana Rais Magufuli.
Halima Mdee amesomewa mashtaka yake na wakili mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa.Imedaiwa, Julai 3, mwaka huu katika ofisi za Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa Wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, alimtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli, kuwa "anaongea hovyo anatakiwa afungwe breki".
Katuga aliongeza kudai kuwa, kitendo kile kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mdee anayetetewa na jopo la mawakili watano, likiongozwa na wakili Peter Kibatala amekana tuhuma hizo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.Mahakama imemtaka Mdee kusaini ahadi ya sh. milioni 10 pamoja na wadhamini wawili ambao pia wamesaini ahadi ya kiasi hicho cha fedha.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika kwa kuwa bado wanasubiri taarifa muhimu za kisayansi, picha za video pamoja na maelezo ya mashahidi muhimu.  
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 7, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.