Habari za Punde

MEYA WA JIJI LA DARA ES SALAAM, ISAYA CHARLES ATEMBELEA BANDA LA PROPERTY INTERNATIONAL

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Issaya Mwita na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta wakitazama ramani ya miradi ya makazi inayojengwa katika eneo la Kigamboni na Kampuni ya Internatinal Property walipotembelea banda la Kampuni hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Saleh Omar Saleh.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Charles (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Property International, baada ya kutembelea Banda hilo katika maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Sabasaba jijini leo mchana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu baadhi ya wateja waliofika Banda lao viwanja vya Mwalimu Nyerere, huku akiwa na baadhi ya Tuzo walizopata katika maonyesho hayo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International, Abdul Haleem (kushoto) na Msanii wa muziki wa kughani,Mrisho Mpoto wakipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya wateja katika Banda hilo.
 Kivutio kingine katika Banada hili ni huyu Jamaa aliyejigeuza Sanamu, ambaye watu wamekuwa wakilipa buku kwa ajili ya kujaribu kumtekenya ili aweze kucheka lakini waaapi, jamaa kaganda tu kama sanamu bila kucheka wala kuongea. Hapa jamaa akijitahidi kumtekenya lakini cha ajabu anatekenya yeye na anacheka yeye,wameshindwa watu kibao, hapa kwani wanasema ukimtekenya na akacheka basi unarudishiwa buku lako. Karibu Banda la PROPERTY INTERNATIONAL ujionee maajabu haya.
 Mfanyakazi wa Kampuni hiyo, Neema Davd, akifurahi na wateja wake baada ya kuwahudumia.
 Bosi wa Dar Zoo,akipiga picha na mtu sanamu huyo nje ya Banda hilo
 Wakimshangaa sanamu huyo.
 Wananchi wakipiga picha za kumbukumbu katika Banda la Property.
Wengi hawakutaka kupitwa kwani selfie pia zilihusika ili kupata kumbukumbu ya huyu mtu muhimu Mzee wa 'Sizonje'.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.