Habari za Punde

PROPERTY INTERNATIONAL YAENDELEA KUTOA ELIMU YA UMILIKI WA VIWANJA KWA WANANCHI MAONYESHO YA SABASABA

 Muonekano kwa nje Banda la Propert International katika Maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo kwa mwaka huu yameongezwa siku ambapo yatamalizika Julai 13 badala ya Julai 8.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Property International, wakiwa bize kuwahudumia wateja wao waliofika kutembelea Banda lao la Maonyesho katika Maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi waliofika katika Banda hilo wakipata maelezo kuhusu viwanja vinavyouzwa na kampuni hiyo, ambavyo vinakuwa vimepimwa tayari huku vikiwa na hati pamoja na miundombinu.
Kwa wanaohitaji kumiliki viwanja hivyo wanaweza kutoa Cash ama kwa mkopo baada ya kuunganishwa na moja kati ya Benki washirika na Kampuni hiyo ambapo kila Benki inakuwa na kiwango chake cha asilimia za kulipia kati ya mteja na Benki hiyo.
Property International ni Kampuni ya kukopesha na kuuza Viwanja, ambapo pia hutumia taratibu za Kibenki kwa malipo ya mkopo katika Benki washirika zisizopungua tano (5).
Benki hizo ni pamoja na PBZ, inayotoa asilimia 80 ya mkopo na marejesho yake ni ndani ya miaka mitatu (3), DCB, pia inatoa asilimia 80 ya mkopo  na narejesho yake ni ndani ya miaka mitano (5) AMANA BANK, inatoa asilimia 80 ya thamani ya kiwanja chako kwa muda wa kuanzia miezi 18, Mteja unahitajika kufungua akaunti na kufanya malipo ya awali ya asilimia 20 ya thamani ya Kiwanja na baada ya hapo Benki itakuwezesha kukupa asilimia 80 ya mkopo wako na marejesho yake ni kuanzia mwaka mmoja au mmoja na nusu, TPBB (Benki ya Posta) wao wanatoa asilimia 95 ya thamani ya Kiwanja chako, ndani ya wiki mbili mpaka tatu wanakuwa tayari wamekuingizia mkopo wako na unalipa mkopo wako ndani ya miaka mitatu (3) na CRDB
 Wananchi wakiendelea kupata maelezo........

Viongozi wa Property wakielekezana jambo katika banda lao
 Baadhi ya wananchi wakiangalia ramani za nyumba na miradi iliyofanywa na kampuni hiyo.
 Wateja wakiendelea kuapata maelezo.
 Mfanyakazi wa Propety, Neema David, akifafanua na kutoa mchanganuo wa mikopo ya benki na marejesho yake kwa mteja, akianza na kumfahamisha kuhusu Kampuni yao, ''Property International ni Kampuni ya kukopesha na kuuza Viwanja, ambapo pia hutumia taratibu za Kibenki kwa malipo ya mkopo katika Benki washirika zisizopungua tano (5).
Benki hizo ni pamoja na PBZ, inayotoa asilimia 80 ya mkopo na marejesho yake ni ndani ya miaka mitatu (3), CBA, pia inatoa asilimia 80 ya mkopo  na narejesho yake ni ndani ya miaka mitano (5) AMANA BANK, inatoa asilimia 80 ya thamani ya kiwanja chako kwa muda wa kuanzia miezi 18, Mteja unahitajika kufungua akaunti na kufanya malipo ya awali ya asilimia 20 ya thamani ya Kiwanja na baada ya hapo Benki itakuwezesha kukupa asilimia 80 ya mkopo wako na marejesho yake ni kuanzia mwaka mmoja au mmoja na nusu, TPBB (Benki ya Posta) wao wanatoa asilimia 95 ya thamani ya Kiwanja chako, ndani ya wiki mbili mpaka tatu wanakuwa tayari wamekuingizia mkopo wako na unalipa mkopo wako ndani ya miaka mitatu (3) na CRDB''
 Maelezo yakiendelea......

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.