Habari za Punde

ROONEY APIGA BAO LA VIDEO TAIFA, SHABIKI AWATOKA ASKARI NA KUMKUMBATIA UWANJANI

 Mshambuliaji wa Everton,Wayne Rooney,akijiandaa kupiga mpira uliozaa bao la kuongfoza kwa timu yake, wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki,uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Everton ilishinda mabao 2-1.
 Shambuliaji wa Everton, Aaron Lennon (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Gor Mahia, Mussa Mohammed,wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki,uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa Everton,Wayne Rooney, akipongezwa na wachezaji wenzake, baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza.
 Gooooooooo, Bao la pili la Everton....
 Mshike mshike.....
 Askari wakionekana kujaribu kumfikia kijana bila mafanikio....
 Kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, akimkumbatia mchezaji wa Kimataifa Wayne Rooney, baada ya kufanikiwa kupenya katikati ya msitu wa Askari waliokuwa wakishangaa kuangalia mpira na kusahau majukumu yao, ambapo kijana huyo aliingia hadi katikati ya uwanja na kufanikiwa kumkumbatia Rooney wakati mpira ukiendelea. Hata hivyo dakika chache baadaye lilitoka tangazo kuwa kijana huyo aachiliwe.
Mshambuliaji wa Everton,Wayne Roone,akirajibu kumtoka beki wa Gor Mahia, Mussa, Mohammed, wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki,uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
****************************************

NA WAMJW-DAR ES SALAAM
UONGOZI wa timu ya mpira wa miguu ya Everton kutoka nchini Uingereza imeridhishwa na huduma inayotolewa kwa wagonjwa  wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo mabusha na matende hapa nchini.
Hayo yamezungumzwa na mmoja wa viongozi wa Everton Bw. Darren Griffiths ambao ni washiriki katika kuchangia huduma ya magonjwa hayo hapa nchini  ambaye ameongozana na timu yake ili kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Gor Mahia kutoka chini Kenya.
“Tunayo furaha kuona wagonjwa wengi waliokuwa wanaumwa mabusha na metende nchini Tanzania kwa sasa wamepona kabisa na tunahaidi kuwa na Wizara ya afya bega kwa bega katika kutokomeza magonjwa haya” alisema Bw. Darren Griffiths
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt.  Vida Mmbaga amesema kuwa kutokana na ushiriki wa Everton katika kuchangia utoaji wa Huduma ya kutibu ugonjwa huo wamefanikiwa kupata ujuzi wa upasuaji hasa kwa wagonjwa wa mabusha na matende hapa nchini.
Aidha Dkt. Vida  amesema kuwa Serikali ikishirikiana vyema na wananchi na mashirika mbalimbali ya afya magonjwa hayo yatatokomea kwa kiasi kikubwa hapa nchini mpaka kufikia mwaka 2025.
Mbali na Hayo Dkt. Vida amesema kuwa anawashukuru watu wa Everton kwa kupitia ushirikiano wao katika sekta ya afya kwa kutoa huduma  pamoja na mafunzo kwa wataalamu ambapo imesaidia kuwafanyia upasuaji wagonjwa  elfu moja.

Kwa upande wake Bw. Yahya Ally Kidege mkazi wa pugu stesheni amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwajali wananchi wake kwani amepata upasuaji wa ugonjwa wake wa busha na amepona kabisa kwan alikua na ugonjwa huo takribani miaka 20.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.