Habari za Punde

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 57 YA UHURU WA CONGO ZAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) na Balozi wa Congo nchini Tanzania, Jean-Pierre Mutamba, wakigonganisha Glasi ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya sherehe za miaka 57 ya Uhuru wa Congo, zilizofanyika nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, jana usiku. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Balozi wa Congo nchini Tanzania, Jean-Pierre Mutamba, akizungumza wakati akisoma hotuba yake katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 57 ya Uhuru wa Congo, zilizofanyika nyumbani kwa Balozi huyo jijini Dar es Salaam, jana usiku. Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) ni Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Mambo ya Nje, Suleiman Saleh.
 Waziriwa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) na Balozi wa Congo nchini Tanzania, Jean-Pierre Mutamba, wakifurahia jambo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 57 ya Uhuru wa Congo, zilizofanyika nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kushoto) na Balozi wa Congo nchini Tanzania, Jean-Pierre Mutamba, kwa pamoja wakikata Keki ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya sherehe za miaka 57 ya Uhuru wa Congo, zilizofanyika nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam.
 Keki ya sherehe hizo
 Baadhi ya Wakongo wakiimba wimbo wa Taifa katika sherehe hizo.
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hizo wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea jukwaani katika maadhimisho hayo.
 Mwanamuziki wa Kimataifa, kutoka Congo, Ferre Gola, akitoa burudani katika sherehe hizo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa pili kushoto) akicheza muziki na mwanamuziki Ferre Gola, wakati wa sherehe hizo.
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hizo wakibadilishana mawazo.
Wanamitindo wakipita jukwaani kutoa shoo la onyesho la mavazi wakati wa sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.