Habari za Punde

TEMEKE YAWANASA VIJANA WANAOSUMBUA KWA UPORAJI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto akiwaonesha wanahabari watuhumiwa wa makosa mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.
******************************************
JESHI la 
Polisi Mkoa wa Temeke limewatia mbaroni wahalifu wa makundi ya ukabaji na uporaji nyakati za usiku na sehemu za fukwe wilayani Temeke, pamoja wanafunzi watoro wakiwemo na wazazi wao.
Kwa mujibu wa kamanda wa mkoa huo Gilles Muroto watuhumiwa wanaoshikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa umri wao ni kati ya miaka 12-25, na kwamba opresheni hiyo ilikamata watuhumiwa wa uhalifu 8 kutoka Mbande na wengine 8 kutoka Chamazi wilayani humo.
Hata hivyo wahalifu hao walikiri kuwa makundi na vishawishi ndio huwasababishia kufanya matukio hayo kwa kutumia visu na mapanga kwa kupora pochi za kina mama kuchukua simu pamoja na fedha.
Kamanda Muroto pia alikemea utoro wa wanafunzi na kutaka wazazi kurejesha watoto wa mashuleni na kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake ya msingi katika kupata elimu.
Nae mzazi Zuhura Hamza alisema watoto wenyewe ndio hawasikii na hawataki kusoma na kwamba wamejitahidi kadri ya uwezo wao lakini hawajapata suluhu la tatizo hilo hivyo akiomba msaada kwa wakuu wa shule.
Kamanda Muruto alitoa wito kwa wazazi wawahimize watoto kwenda shule, kwani watoto wamezagaa mitaani na kujiingiza katika makundi mabovu kama ya madawa ya kuevya, uporaji, uvuataji bangi na sigara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke Afande Gilles Muroto akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwashikilia watuhumiwa wa makundi ya ukabaji na uporaji nyakati za usiku na sehemu za fukwe wilayani Temeke, pamoja na wanafunzi watoro wakiwemo na wazazi wao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto akiwaonesha wanahabari watuhumiwa wa makosa mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.